Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Ishirini (20)
Miongoni mwa vitu ambavyo huwa sivipendi, ni mtu kuanza kunihoji kuhusu maisha yangu bila kuangalia tupo kwenye mazingira gani.
Dakika chache tu nilizosimama na msichana huyo, alikuwa ameniboa vya kutosha na japokuwa mwanzo nilikuwa naficha hisia zangu, safari hii niliweza kumuonesha waziwazi kwamba sipendezwi na maswali yake.
“Aah! Basi kuna mtu nilitaka kukuulizia habari zake lakini nimeshamuona, bye!” nilisema huku nikigeuka na kuanza kupiga hatua ndefundefu, hata sikuwa naelekea wapi ndani ya hospitali hiyo ya Muhimbili kwa sababu sikuwa mwenyeji.
Nadhani bado alikuwa hajatosheka, akanikimbilia na kunisimamisha, nikamgeukia huku nikiwa nimekunja ndita.
“Mbona umekasirika?”
“Mwenzio nina mgonjwa nimekuja hapa kwa matatizo lakini wewe hujali unachojua ni kunisanifu tu.”
“Aah! Jamani basi nisamehe mbona sikuwa na lengo lolote baya,” aliniambia kwa sauti ya upole, sikutaka hata kumtazama usoni, akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya kisasa kwenye gauni la kazi alilokuwa amevaa.
“Naomba nitafute baadaye kama hutajali, naona sasa hivi haupo sawa,” alisema kwa upole huku akinitazama machoni, nikaichukua simu harakaharaka na kuandika namba yangu kisha nikamrudishia.
“Nisamehe bwana kama nimekuudhi, nna zawadi yako baadaye naomba nikikupigia simu upokee,” alisema huku akigeuka, nikabaki kumtazama.
Japokuwa alikuwa amevaa yunifomu, ‘nundu’ kubwa iliyokuwa imechomoza upande wa nyuma haikuweza kujificha, nikajikuta navutiwa kuendelea kumtazama.
Akawa anatembea harakaharaka na ni kama alijua kwamba namtazama kwani alipofika mbele kidogo, aligeuka, akanibamba nikiwa namkodolea macho, akacheka na kupotelea kwenye kundi la wagonjwa.
Kwa sekunde chache zile chache nilijikuta nasahau kwa muda kilichonipeleka hospitalini hapo, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kujiuliza sehemu ya kuanzia kwa sababu tayari alishanipotezea ‘taiming’. Nilitamani nimuite na kumwambia ile namba niliyompa nilikuwa nimekosea namba moja kwa makusudi lakini sikuupata muda huo.
Ilibidi niende mpaka kantini kuzuga nikiwa najipanga upya sehemu ya kuanzia, nilipanga nikikutana hata na mlinzi nimuulize sehemu ya kupima Ukimwi. Wakati nikielekea kantini, nilishtuka nikitokea mbele ya kundi kubwa la watu ambao wengi walikuwa wakilia huku wengine wakiwa na huzuni kali, ilionesha kwamba wapo kwenye maombolezo.
Kumbe nilikuwa nimetokezea mochwari, kwa wale wanaofahamu vizuri mazingira ya Muhimbili, watakuwa wanaelewa kwamba mochwari inatazama na kantini ndogo, achana na ile kantini kubwa iliyopo nyuma ya jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Basi sijui kwa nini nilipowapita wale waombolezaji, nilianza kujiona eti na mimi ndiyo tayari nimeshaumwa sana na kukonda kutokana na Ukimwi na sasa mauti yameshanifika kwa hiyo ndugu zangu wapo msibani, kwenye msiba wangu.
Nilijikuta mwili ukitetemeka na kusisimka mno, yaani nilitamani kama siku zirudi nyuma nibadilishe kabisa tabia na kuacha kurukaruka hovyo na wanawake na hata pale inavyotokea hivyo, basi nisiuze tena mechi bali nivae kinga.
Mawazo ya hofu ya kufa kwa ngoma, yalinifanya niendelee kutembea kuifuata ile barabara inayopita kati ya mochwari na kantini, kuja kushtukia nilijikuta nikiwa kwenye geti la kutokea, nikawa najiuliza nimefikaje?
Akili nyingine ilinituma labda niondoke na kurudi nyumbani ili nijipange vizuri siku ya kuja kupima, akili nyingine ikawa inaniambia nikapime hivyohivyo, liwalo na liwe. Lakini mwili ulikuwa ukitetemeka sana nilipokuwa nikifikiria kwenda kupima, vilio vya wale waombolezaji vikawa vinaendelea kusikika kwenye masikio yangu.
Siku za nyuma nimewahi kuwa mtumiaji mzuri wa pombe lakini tatizo langu ni kwamba nilikuwa na kichwa kibovu kwelikweli, yaani bia mbili tatu kichwani zilikuwa zinanifanya nionekane kama nimekunywa kreti zima.
Nilichokuwa naamini ni kwamba pombe zinakupa ujasiri wa kufanya hata yale ambayo ukiwa macho makavu huwezi kuyafanya maana nakumbuka kuna siku nilikunywa na kujikuta namtongoza mwanaume mwenzake nikifikiri ni mwanamke kwani alikuwa mnene, sitasahau fujo zilizoibuka baada ya kitendo hicho.
“Ngoja nikapige bia mbili kwanza ili nipate ujasiri wa kwenda kupima,” niliwaza wakati nikitoka kwenye geti la Muhimbili, nikakatiza kwenye baa moja iliyokuwa jirani na hospitali hiyo.
Kwa kuwa ilikuwa ni siku ya kazi na pombe hazikuwa zikiruhusiwa kunywewa mchana, ilibidi muuzaji anifanyie njama za kuifunga kwenye gazeti na kunipa, akaniambia nikikamatwa yeye hahusiki, basi harakaharaka nikaanza kuigida bia ya kwanza huku bado nikiwa natetemeka.
Haukupita muda, nikawa nimeshaikata, akaniletea nyingine, nikawa naigida kwa kasi na ilipofika nusu, tayari mafaili yalikuwa yameanza kupandana kichwani. Hata sikumbuki kama niliimalizia hiyo bia ya pili au laa, na pia sikumbuki niliondokaje.
Baadaye nilijikuta nimeshafika kwenye kituo cha mabasi cha Faya, jasho likiwa linanitoka kwelikweli, nikawa najiuliza hivi tayari nimeshapima? Sikuwa na majibu. Na kama nimepima, hivi nimepewa majibu kweli? Pia sikuwa na majibu, nikaona isiwe kesi, ngoja nikapumzike kwanza nyumbani maana nilikuwa najihisi kama nimelewa sana.
Nilipanda kwenye daladala na nilipokaa kwenye siti tu, nilipitiwa na usingizi mzito. Nilipokuja kushtuka, tayari gari lilikuwa limefika Sinza kijiweni, kwa lugha nyepesi nilikuwa nimepitishwa kituo, nikashuka huku nikiwa napepesuka na kuingia ndani ya Bajaj, nikamuelekeza dereva kunipeleka nyumbani.
Kwa bahati nzuri alinielewa, tukaondoka mpaka nyumbani, nikamlipa kisha nikaingia ndani. Nilipofungua tu mlango na kuingia ndani, huku pombe sasa zikiwa ndiyo zimekolea kisawasawa, nilisikia mtu akinifuata kwa nyuma. Japokuwa nilikuwa na akili za pombepombe, nilikuwa kumtambua kwamba ni Khazija. Nilipomuona tu, nikaanza kuangua kilio.
“Kwa nini umeniua Khazija? Kwa nini umenipa ngoma?” alishtuka sana kusikia maneno hayo, akafunga mlango kwa funguo na kunisogelea pale kwenye kiti nilipojitupa huku nikindelea kulia kipombepombe.
“Umepatwa na nini wewe?”
“Niachee! Niacheee! Mwanamke muuaji sana wewe,” nilisema kwa sauti ya juu, akazidi kupigwa na butwa, hata sijui kilitokea nini lakini ninachokumbuka, nilimuona akivua kufuli lake. Sikuelewa tena kilichoendelea, nilikuja kushtuka na kujikuta nikiwa juu ya kitanda na Khazija. Hata sikumbuki nguo zangu zilitokaje mwilini.
“Unalia nini sasa, au hutaki nikupe?” aliniuliza huku akiniweka mkao mzuri wa kulamba asali, hata sikumbuki nilimjibu nini, nikajikuta tayari nimezama kwenye bahari ya kina kirefu, nikawa nafanya yangu huku nikiendelea kugugumia kwa kilio cha chinichini ambacho kadiri tulivyokuwa tukiendelea ndivyo kilivyokuwa kinazidi kushuka.
Unajua aliyesema mwanamke siyo mtu wa kushindana naye hakukosea kabisa, yaani kumbadilisha mwanaume mawazo ni jambo la sekunde chache sana, akijua kukupumbaza akili hata kama wewe ni mkuu wa majeshi unaweza kuiingiza nchi kwenye vita bila kutegemea ilimradi tu umfurahishe.
“Nani amekwambia kwamba mimi nimeathirika?”
“Ni mama mwenye nyumba, ameniambia eti wewe unajiuza,” niliropoka hata bila kufikiria mara mbilimbili madhara ya majibu niliyokuwa nampa, naye ni kama alijua kwamba nimefika kwenye kile wazungu wanachoita ‘a point of no return’, basi akaongeza mbwembwe huku akinipiga maswali mfululizo, na mimi nikawa namwaga tu mchele kwenye kuku wengi.
Mpaka kipyenga kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mpambano, nilikuwa nimesahau kabisa ile hofu kubwa niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu kwamba ‘nimeungua’, basi Khazija akawa anaendelea kunipetipeti huku akiniambia kwamba eti mimi ni dume la mbegu niliyekamilika kila idara.
“Lakini Khazija, hebu niambie ukweli mama, hivi kweli wewe huna ngoma?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, hofu ikawa imeanza kurudi upya ndani ya moyo wangu. Basi Khazija alicheka kwa nyodo za kikekike na kunitazama usoni, akawa anajikaza kuzishinda aibu zake za kikekike.
“Hivi ukiniangalia nafanana na mwanamke anayefanya biashara ya ukahaba? Hivi ukiniangalia unaona nafanana na mtu mwenye Ukimwi?”
“Lakini wanasema huwezi kumtambua mwathirika kwa kumtazama kwa macho.”
“Wala usiwe na wasiwasi, mimi nataka tuongozane mguu kwa mguu mpaka hospitalini tukapime, najua umeshalishwa sumu ya hatari mpaka ukaamini kwamba mimi ni mgonjwa.
“Umenikosea nini mpaka nikuambukize virusi kwa makusudi? Au kwa sababu ‘nilijilengesha’ kwako ndiyo unanifikiria mimi ni mwanamke wa hovyo kiasi hicho?” alisema Khazija huku safari hii akiwa ‘siriasi’.
“Niliamua kujilengesha kwako kwa sababu nilikupenda, nakumbuka siku ya kwanza kukuona tulipishana pale dukani lakini sidhani kama wewe uliniona. Lakini pia nimekushuhudia zaidi ya mara tatu ukiwasulubu wanawake watatu tofauti, moyo ukawa unaniuma sana kwa sababu ya wivu.
“Isitoshe mimi ndiyo nilitakiwa niwe na hofu kama hujaniambukiza virusi kwa sababu ndani ya siku chache tu nimekufuma na wanawake watatu tofauti, tena mara zote ulikuwa ‘unauza mechi’ na kibaya zaidi kumbe huwa unakunywa pombe kama hivi, sasa ukilewa si utakuwa unawaparamia mabaamedi hovyohovyo?” alisema Khazija na kunifanya nishtuke sana.
Kikubwa kilichonishtua ni kauli yake kwamba amenishuhudia mara tatu nikiwa naivunjilia mbali amri ya sita na wanawake tofautitofauti, ikabidi nimhoji ili nipate uhakika.
“Mara tatu?”
“Ndiyo, unataka nikupe uthibitisho? Mara ya kwanza ulikuwa na dada mmoja mrefumrefu hivi amejazia ila hajanizidi mimi, mara ya pili ulikuwa na jimama fulani hivi jeupee na mara ya mwisho ulikuwa na mama mwenye nyumba, bisha tena,” alisema Khazija.
Nilishangaa sana kugundua kwamba kumbe alikuwa ananifuatilia bila mwenyewe kujijua, nikashindwa hata kuendelea kumtazama usoni na kujiinamia. Kwa maelezo yake hayo, ilionesha kwamba kumbe siku ile nilipokuja na Nancy pale nyumbani aliniona na alishuhudia kila kitu, siku nilipokuja na Madam Bella, bosi wangu pia alishuhudia kila kitu na kibaya zaidi kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa akitupiga chabo wakati tukibingirishana na mama mwenye nyumba.
“Kama kweli unaogopa virusi kama ulivyokuwa unaniletea uchuro kwa kulia na kudai mimi ndiyo nimekuambukiza, unatakiwa kubadilisha mwenendo wako! Mungu amekujaalia zawadi ya kuwa ngangari kwenye sita kwa sita lakini hii inatakiwa iwe zawadi kwa mwanamke mmoja tu atakayekuwa mkeo na si kugusagusa kila mahali, mimi nakupenda ndiyo maana nakwambia maneno haya.”
“Kwani huwa ukiondoka usiku unaenda wapi?” nilijikakamua na kumuuliza, lengo likiwa ni kupata uhakika kama kweli nipo salama.
“Mimi nafanya kazi ya ‘customer care’ kwenye kampuni ya simu pale Mlimani City, naweza kuingia shift ya usiku hata wiki tatu mfululizo lakini mimi sijiuzi wala siwezi kufanya upuuzi huo, mshahara ninaolipwa unanitosha kuishi maisha yoyote ninayotaka, upo?”
Hiyo ndiyo kauli ambayo hasa nilikuwa naihitaji kutoka kwake, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni huku katabasamu hafifu kakiwa kameanza kuchanua kwenye uso wangu. Kwa maelezo hayo, ile hofu yote niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu, iliyeyuka kama barafu iyeyukavyo juani.
Niliinuka na kwenda kuwasha redio, nikaweka CD ninayoipendaga, yenye nyimbo za kulalia na kuchagua wimbo wa George Michael uitwao Careless Whisper, nikabonyeza kitufe kwenye rimoti ili wimbo huo uwe unajirudia, nikarudi kitandani na kumvaa Khazija ambaye bado alikuwa akiendelea kutoa maneno mazuri ya kuniusia juu ya tabia yangu.
Kwa furaha niliyokuwa nayo, ya kuhakikisha kwamba kumbe hakuwa changudoa kama mama mwenye nyumba alivyoniaminisha, niliamua kuingia upya uwanjani, nikiwa na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya huku muziki laini uliokuwa ukipiga kwenye redio yangu kubwa ukizidi kunidatisha.
Akiwa anaendelea kuongea kwa upole, nilianza kumfanyia vituko vya hapa na pale na kusababisha kauli zake ziwe zinakatakata, haikuchukua muda tayari naye alishaanza kunionesha ushirikiano, safari hii ikawa zamu yangu.
Nilimuweka sawa, nikapitisha mikono yangu kwa nyuma yake na kuukamata mlima wake kwa staili fulani hivi ya kipekee sana, nikamuona akijikunjakunja kama nyoka aliyemeza mbuzi mzima, nikaweka mwiko kwenye chungu na kuanza kufanya kama nasonga ugali hivi!
Nadhani kilikuwa kitu kipya kabisa kwake kwani miguno aliyokuwa akiitoa haikuwa ya kawaida, akawa anahema kama anataka kuzama kwenye maji ya kina kirefu, basi nikazidisha mbwembwe huku nikimtazama usoni jinsi alivyokuwa akibadilikabadilika kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Ilifika mahali akaanza kuweweseka kama mtu aliyepo kwenye njozi, mara azungumze hili mara azungumze lile, basi ilikuwa ni tafrani ya aina yake.
Haukupita muda mrefu akatangaza kuiona theluji iliyopo juu kabisa ya Mlima Kilimanjaro unaoongoza kwa kupendwa na watalii, sikutaka kumchosha sana, na mimi nikaongeza spidi ya kukwea juu ya mlima na muda mfupi baadaye, na mimi niliiona theluji, nikamuachia na kila mmoja akadondokea upande wake.
Baada ya kama dakika kumi hivi kupita, aliinuka na kuja kunilalia kifuani kwangu, akazungumza jambo ambalo sikulitegemea kabisa kutoka kwake.
“Nataka unioe niwe mke wako! Mi nakupenda mwenzio na nakuahidi nitakupenda siku zote za maisha yako na nitakubadilisha, sasa hivi unahangaika hovyo na wanawake kwa sababu hujampata mtu anayeweza kukubadilisha,” alisema kwa hisia za hali ya juu huku akinibusu kila baada ya sekunde kadhaa.
Japokuwa wakati naingia nilikuwa nimelewa chakari, ‘dawa’ aliyonipa Khazija ilinifanya hata nisikumbuke kama nilikuwa nimekunywa. Nilibaki namkodolea macho nikiwa ni kama siamini kama kile alichokuwa anakisema kimetoka kwenye kinywa chake.
Nilieleza mara ya kwanza kwamba japokuwa nilikuwa na muda mfupi tangu nifahamiane na Khazija, alikuwa na uzuri fulani wa kipekee ambao ama kwa hakika ulikuwa ukinichanganya sana kichwa changu, hasa jinsi alivyokuwa amegawanyika nyonga yake na kubeba mzigo wa kutosha upande wake wa nyuma.
Sikuwa na malengo ya kuoa lakini kwa jinsi Khazija alivyokuwa amenichanganya kichwa changu kwa penzi motomoto alilokuwa ananipa, nilijikuta nikishawishika.
“Kwa hiyo unataka nikuoe?” niliuliza nikiwa hata sijui nataka kujibiwa nini kwa sababu tayari alikuwa amefunguka kila kitu.
“Nakupenda sana mwenzio, mimi ni mgumu sana kujirahisi kwa mwanaume, wapo watu walikuwa wanakuja kunifuata kazini na magari yao ya thamani lakini hakuna aliyewahi kunivutia lakini tangu nilipokuona wewe, nimejikuta nikikupenda na kuridhika mno na wewe, hata sijui moyo wangu utahitaji nini cha ziada nikiwa mkeo,” alizidi kulalama Khazija kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba yaliyotukuka.
“Lakini Khazija, mimi mwenzio nina... nina...” nilitaka kusema jambo lakini maneno yakawa yanaishia ndani kwa ndani, nilitaka ‘nimchane’ ukweli kwamba mwenzake sijatulia hata kidogo na sijui kama nitaweza kutulia japokuwa nilikuwa ‘nimemuelewa’ sana.
Kabla hata sijamalizia kauli yangu, alidakia juu kwa juu na kuniambia kwamba anajua kwamba sijatulia lakini amenipenda hivyohivyo na atahakikisha ananibadilisha. Aliposema hivyo, akili zangu zilienda kwa Ruqaiya, nikajiuliza kweli nawezaje kumuacha mwanamke kama yule? Yaani raha zote zile tulizopeana halafu ghafla eti nimwambie mimi na wewe basi, nimepata mchumba? Niliona ni jambo lisilowezekana.
Nilimfikiria Nancy, jinsi alivyokuwa akinipenda na kujituma kwa moyo wake wote kuhakikisha nafurahi, akafikia hatua mpaka ya kurudi nyumbani kwao usiku wa manane, naanzaje kumwambia mimi na yeye basi?
Yote tisa, kumi nilikuwa namfikiria bosi wangu, Madam Bella, nawezaje ‘kumchomolea’ kirahisi eti kisa nimepata mwanamke anayetaka tuoane na kuishi kama mume na mke?
“Haiwezekani!” nilijikuta nimetamka, Khazija akashtuka akiwa ni kama haamini alichokisikia.
“Haiwezekani! Haiwezekani kabisa,” nilisema kwa sauti ya juu huku nikiwa najitoa kwenye mikono yake, akazidi kupigwa na butwaa.
“Umepatwa na nini?”
“Sijapatwa na chochote, mimi sijajiandaa kuoa kwa sasa, kwanza mimi bado mdogo.”
“Hujajiandaa kivipi? Mdogo kwani una umri gani wewe?” Khazija alitaka kunibana kwa hoja lakini nazidi kumkwepa kwa kusisitiza kwamba sikuwa tayari kumuoa.
“Kwa hiyo nimefanya makosa kukupenda?”
“Hapana, siyo hivyo mpenzi wangu, wala hujakosea chochote na mimi napenda tuendelee kuwa wapenzi lakini hilo suala la ndoa naomba tuliache kwanza,” nilisema, nikamuona akibadilika, uso wake ukajawa na huzuni isiyoelezeka.
Ilibidi nianze kazi ya kumbembeleza Khazija, nikamwambia asiwe na wasiwasi sina lengo lolote la kumuacha bali nataka kwanza tufahamiane kwa kina kisha mambo mengine yote yatafuatia, kwa mbali nikamuona kama ameanza kuelewa ‘saundi’ zangu.
Basi siku hiyo aliniganda kuliko kawaida, ikawa kila baada ya muda mfupi ananipeleka ‘msambweni’ mpaka nikawa hoi bin taaban, hata sikumbuki nililala saa ngapi, ninachokumbuka nilikuja kuzinduka baada ya kusikia jogoo akiwika kuashiria mwanzo wa siku mpya, mapambazuko!
Nilishtuka kugundua kwamba sikuwa nimelala peke yangu, nilipogeuka pembeni yangu, nilimuona Khazija akiwa amelala fofofo, wote tukiwa watupu na tukiwa tumejifunika shuka moja. Nilijikuta nikitamani kumkumbatia Khazija, nikawa najiuliza ilikuwaje mpaka akalala na mimi? Hajaenda kazini usiku kama kawaida yake?
Nilipomkumbatia, ni kama na yeye alizinduka nusunusu kutoka usingizini, kwani naye alinikumbatia na kunibusu kisha akajilaza kwenye kifua changu. Baadaye aliamka, akanibusu kwa mahaba mazito na kuniuliza nimeamkaje, nikawa nachekacheka tu mwenyewe.
INAENDELEA
No comments