Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Ishirini na Tatu (23)

hadithi nzuri ya kivuruge wa tandale
“Huu mchezo wako wa kubadilisha wanawake kama nguo, mwenyewe unaona ni ujanja sana si ndiyo?” aliniuliza swali ambalo sikulitegemea.

“Hamna, wala mimi sipo hivyo sema unakuwa unanihisi vibaya tu,” nilianza ‘saundi’ zangu kama kawaida. Akaniuliza kwa nini nasema hivyo wakati ushahidi wa kila kitu ulikuwa wazi? Nikamwambia kwamba Ruqaiya hakuwa mpenzi wangu kama yeye au Khazija walivyohisi bali alikuwa ndugu yangu.

“Ndugu yako ndiyo mnajifungia kutwa nzima ndani, baadaye mnatoka kwenda kuoga pamoja? Huo undugu gani?” alinibana kwa maswali, nikakosa cha kujibu, akaniuliza pia kuhusu Khazija.

“Tumezoeana tu bwana wala hakuna chochote kinachoendelea, nashangaa yeye anaanza kuniletea wivu wa kimapenzi,” nilidanganya waziwazi, akawa ananikazia macho usoni.

“Lakini kwa nini unanibana kwa maswali namna hiyo, kwa nini usinipe hata pole mwenzako nilitaka kuchinjwa leo?” nilisema huku nikimgusa kijanja kwenye maeneo ambayo nilikuwa najua kwamba lazima mazungumzo yatabadilika.

Nilichokihisi ndicho kilichotokea, alikatisha mazungumzo yake na kunivaa mzimamzima, tukagusanisha ndimi na kuanza kuelea kwenye bahari ya huba. Mkono wake mmoja aliupeleka kwa ‘mkuu wa kaya’ na kuanza kuzungumza naye kwa lugha ya vitendo, hali iliyosababisha nisahau kwa muda kilichotokea kwa Khazija.

“Unajua kwamba nakupenda ndiyo maana unanitesa kwa kubadilibadili wanawake kama nguo,” alisema kwa sauti iliyotokea kwenye matundu ya pua zake, nikawa najibu kwa kugugumia tu kama dume la njiwa, sijui alinipinduaje bwana, nikajikuta nipo kwa chini yeye juu, tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.

“Nisamehe,” nilinguruma kwa sauti ya kiume, akatabasamu bila kujibu kitu na katika hali ambayo sikuitegemea, alishika kipaza sauti kwa bashasha za hali ya juu na kuanza kughani mashairi matamu, kuonesha kwamba msamaha wangu umepita, nikawa nazidi kugugumia tu ndani kwa ndani.

Baada ya kumaliza kughani ubeti wa kwanza, alimkamata ‘mkuu wa kaya’ na kumuelekeza sehemu ya kwenda, naye akatii bila shuruti.

Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni mwendelezo wa burudani na kiukweli mwili wangu ulikuwa umechoka mno kiasi kwamba baada ya mama mwenye nyumba kutangaza kuiona theluji ya Mlima Kilimanjaro, sikupoteza muda na mimi nikatangaza kufika mwisho na muda huohuo, nilipitiwa na usingizi mzito.

Hata sikumbuki mama mwenye nyumba aliondoka saa ngapi lakini nilipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni karibu saa nane za usiku. Bahati mbaya ni kwamba nilikuwa nimemfungia Khazija ndani kwa muda wote huo.

Harakaharaka niliinuka kitandani, kumbe hata mlango wangu sikuwa nimeufunga, nikatoka huku macho yakiwa yamefumbuka nusu kutokana na kuzidiwa na usingizi. Sijui nini kilichokuwa kimetokea kwani nilipokaribia tu mlango wa Khazija, nilisikia akiniita kwa jina langu.

“Naomba nifungulie mlango, sijui mshenzi gani amenifungia kwa nje,” alisema Khazija kwa sauti ya juu, nikasita kidogo kwa sababu bado mimi na yeye hatukuwa tumefikia muafaka kwenye tatizo lililokuwa limetokea mpaka akataka kunichoma kisu.

“Najua una wasiwasi na mimi, wala siwezi kukufanya chochote, hasira zangu zimeshaisha na isitoshe nahitaji kuzungumza na wewe,” alisema Khazija kwa upole, nikashawishika kwenda kumfungulia huku moyoni nikijiambia kwamba liwalo na liwe.

“Wewe ndiye uliyenifungia mlango, si ndiyo?”

“Mimi? Hapana.”

“Kama siyo wewe ulikuwa unakuja mlangoni kwangu muda huu kufanya nini?”

“Nilitaka kuhakikisha kama upo salama,” nilimdanganya, akanitazama kwa macho yaliyojaa uchovu kisha akanisogelea mwilini, na mimi nikawa najihami kwani kwa kitendo alichonifanyia saa chache zilizopita kilinifanya niwe naye makini sana.

“Lakini kwa nini umenifanyia uliyonifanyia mpenzi wangu? Ina maana sikuridhishi baba?”

“Hapana siyo hivyo Khazija.”

“Sasa kwa nini ulale na mwanamke mwingine kwenye kitanda unacholala na mimi, tena muda mfupi baada ya mimi kukupa kila ulichokuwa unakitaka mpenzi wangu?” alisema Khazija huku akinikumbatia, machozi mengi yakaanza kumtoka na kuchuruzika mpaka kwenye shingo yangu.

Kimsingi nilimuonea huruma, na mimi nikamkumbatia, ukichanganya na kile kibaridi cha usiku ule, nilijikuta nikitamani kuendelea kumkumbatia, akawa anazidi kulia huku maneno mengi ya kunilaumu yakimtoka.

“Lakini Khazija, mimi nimeshakwambia kwamba hakukuwa na jambo lolote baya bali wewe umehisi vibaya, nakupenda sana na mimi siyo mchoyo wa fadhila kiasi hicho, kwa nini nikutese wakati nakupenda,” kidume nilianza kumwaga sera.

Miongoni mwa masuala ambayo nilikuwa najiamini kwamba niko fiti, ilikuwa ni kwenye suala zima la kuwadanganya wanawake. Nilimpanga kwa maneno matamu, akawa anaendelea kulia, ikafika mahali na mimi nikamgeuzia kibao.

“Hata kama ingekuwa ni kweli nimekusaliti, ndiyo utake kunichoma kisu Khazija?”

“Hapana, nisingeweza ila nilitaka tu kukutishia.”

“Muongo, kunitishia kivipi wakati ulikuwa ‘serious’ kabisa unataka kuniua?”

“Hapana, siwezi kufanya hivyo. Hata kuku tu sijawahi kuchinja, ndiyo itakuwa wewe kipenzi changu, mwanaume wa roho yangu? Siwezi! Siwezi,” alisema Khazija, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni.

Unajua kwa kipindi kirefu mimi nilikuwa najifanya mjanja lakini kwa Khazija nilikuwa nimegonga mwamba. Na yeye alikuwa fundi wa kuzungumza kiasi kwamba akiamua kukupangia maneno, huwezi kupinga chochote.

“Mimi na wewe tumeshapanga mambo mengi sana mume wangu, hayo yote unataka yavurugike kwa hiki kilichotokea? Naomba nisamehe kama nimekukosea na wewe nimekusamehe,” alisema huku akiniachia maana bado alikuwa amenikumbatia, akataka anivutie chumbani kwake.

“Basi tutaongea vizuri kesho asubuhi kabla sijaenda kazini,” nilimwambia lakini hakutaka kunielewa kwa chochote, akanivutia ndani. Kwa kuwa nilikuwa nimepumzika kwa zile saa chache nilizolala, niliona basi isiwe kesi.

“Basi naomba nikafunge mlango,” nilimwambia, akaniambia nisiwe na wasiwasi, anaenda kufunga yeye mwenyewe. Basi sikuwa na ujanja, ilibidi nitulie. Akaenda chumbani kwangu na kufunga vizuri milango, akarudi akiwa na funguo.

“Mbona kitanda chako kimevurugika namna ile, ulikuwa umelala na nani?”

“Nitalala na nani tena kama wewe mke wangu hunitaki?” nilimwambia, akanisogelea taratibu pale kitandani na kujilaza pembeni huku akijinyonganyonga umbo lake zuri kimitego, akawa ananitazama kwa macho yaliyokuwa yamebeba ujumbe mzito huku mikono yake laini ikipita taratibu kwenye mwili wangu.

Kile kibaridi kilichonipiga pale nje wakati nazungumza naye, kilinifanya niwe na shauku ya kumsogeza mwilini mwangu, nikamuinua taratibu na kumsogeza kwenye kifua changu, tukawa tunatazamana.

“Unajua wewe ni ‘daktari’ mzuri sana lakini tatizo lako unazingua.”

“Nazingua nini tena jamani?”

“Unapenda sana wanawake, yaani wewe kivuruge haswaa, na hilo jina limekukaa kisawasawa,” alisema huku akitabasamu, mkono mmoja akiwa anaupitisha taratibu kuelekea katikati ya miguu yangu.

“Na wewe tatizo lako una hasira sana, mwanamke gani anamshikia mumewe kisu? Nitakuwa sikuoi, ohooo!” niliongeza kimasihara, akacheka sana na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumegusanisha ndimi zetu.

Nafsi ilikuwa inataka lakini mwili ulikuwa unakataa, nikaona ngoja nijifosi kidogo kwa sababu ili kumtuliza Khazija, ilikuwa ni lazima nifanye jambo ambalo lingemfurahisha. Kwa bahati nzuri, kwa sababu tayari nilikuwa nimepumzika vya kutosha, sikupata tabu sana kuliwasha gari, ukichanganya na mbwembwe za Khazija usiku ule, basi haikuchukua muda tukawa tayari mchezoni.

“Nakupenda sana mume wangu, ukinisaliti tena nitakuua,” alisema Khazija wakati nikiendelea kupiga naye mbizi kwenye bahari ya huba yenye kina kirefu.

“Ukiniua na mimi nitakuua,” nilisema huku nikiendelea na kazi, akacheka sana na kuniambia kwamba hawezi kuniua bali ananitania isipokuwa nikiendelea kumsaliti, kweli ataenda kuniroga kama alivyoniahidi tangu awali.

Haikuwa mara ya kwanza kwa Khazija kuzungumza kauli hii kiasi cha kufanya nianze kuamini kwamba kweli anaweza na mawazo hayo kichwani mwake, hasa ukizingatia kwamba kwao Pemba, kunasifika kuwa na waganga wenye nguvu kubwa za kishirikina.

Basi hata sijui tulilala saa ngapi, nilikuja kuzinduka alfajiri na kujikuta nikiwa kwenye kifua cha Khazija, tena akiwa amenikumbatia kisawasawa.

Nilichokigundua ni kwamba Khazija alikuwa ananipenda sana na kamwe hakuwa tayari kunipoteza kwa namna yoyote ile kwa sababu, kwa mwanamke mwingine isingekuwa rahisi kulala tena na mimi mpaka asubuhi baada ya purukushani iliyotokea usiku uliopita.

Yaani kama ungetuona, usingeamini kwamba ni sisi ndiyo tuliojaza watu nje ya nyumba hiyo usiku uliopita, baada ya Khazija kutaka kunichoma na kisu baada ya kunifumania.

“Hivi nashindwa nini kutulizana na mtoto mzuri kama huyu? Kwanza kiumri huyu ndiyo rika langu, hivi nimerogwa nini?” nilijiuliza wakati nikijitoa taratibu kwenye mikono yake maana nilitaka nikaanze kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini.

Wakati nikitaka kujitoa, alizinduka kutoka usingizini, akazidi kunikumbatia huku akinimwagia mvua ya mabusu. Hata sijui alitumia ujanja gani bwana, nikashtukia ‘mkuu wa kaya’ akikurupuka kutoka kwenye himaya yake, naye wala hakuwa na hiyana, akampa kile alichostahili na kusababisha kijasho chembamba kianze kunitoka asubuhi hiyo.

“Usiende kazini mpenzi wangu, waambie kwamba unaumwa na leo tushinde wote,” aliniambia lakini nikamkatalia katakata. Alinielewa, akanibusu tena na kuniruhusu nikajiandae.

Nilitoka nje huku miguu ikiwa haina nguvu kabisa kiasi cha kunifanya niwe napepesuka kama mlevi wa gongo. Awali nilidhani ni hali ya muda tu lakini huwezi kuamini, niliendelea kutetemeka miguu hata baada ya kuoga.

“Hata iweje lazima niende kazini,” nilisema huku nikijikakamua kiume, nikafungua kabati na kutoa suruali niliyokuwa naipenda. Cha ajabu, nilipoivaa, eneo la kiunoni kulibaki na uwazi mkubwa ulionishtua.

Ni suruali hiyo ndiyo niliyokuwa naivaa mara kwa mara na siku zote ilikuwa inanibana, iweje leo inipwelepwete? Ilibidi nijitazame vizuri, nikashtuka mno kugundua kwamba nilikuwa nimekonda sana, yaani kiuno kilipungua mno na kunifanya niwe kituko kwa ile suruali niliyokuwa nimeivaa.

Cha ajabu zaidi ni kwamba nilikuwa nimekonda ghafla kuanzia kiunoni kushuka chini.


Hapohapo nilianza kusikia kizunguzungu kikali, miguu ikawa inatetemeka na nikaishiwa nguvu. Nilishindwa kufanya chochote na bahati nzuri ni kwamba Khazija alikuja chumbani kwangu kwa lengo la kuniaga vizuri, akanikuta nikiwa nimelala kwenye kochi nikiwa hoi.

“Vipi tena?”

“Hata siele...wi!”

“Unaumwa?”

“Ha..pa..na ila mwili hauna nguvu,” nilisema, naye akawa ni kama amechanganyikiwa. Alitoka mbiombio na kwenda kutafuta usafiri, muda mfupi baadaye alirejea akiwa na dereva Bajaj, wakasaidiana kunibeba na kunitoa nje.

“Duh! Mbona umekuwa mwepesi kiasi hiki mwanangu?” alisema yule dereva teksi wakati akinisaidia kuingia kwenye Bajaj, sikuwa na cha kumjibu, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea hospitali ikaanza.

Kwa jinsi hali niliyokuwa nayo, tulienda moja kwa moja mpaka Hospitali ya Mwananyamala ambapo tulipofika tu eneo hilo la hospitali, nilizidi kuzidiwa, nikawa natapika huku mwili ukiwa hauna nguvu kabisa. Sikuelewa tena kilichoendelea.

Nilipokuja kupata akili zangu nilijikuta nikiwa nimelala kitandani huku dripu ikitiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yangu. Khazija alikuwa amekaa pembeni yangu huku akiwa amejiinamia, muda mfupi baadaye akaingia dokta na kuanza kunipimapima.

Japokuwa nilikuwa na uwezo wa kuona kila kilichokuwa kinaendelea, sikuwa na uwezo wa kujibu chochote, nikamsikia daktari akimuuliza Khazija ana uhusiano gani na mimi.

“Ni mume wangu!”

“Mh! Ana wake wangapi au ni wewe peke yako?”

“Ni mimi peke yangu, kwani vipi dokta?” aliuliza Khazija lakini hakumjibu chochote, akaendelea kunipimapima na baadaye, alitoka na kutuacha na nesi aliyekuwa amekaa pembeni akiendelea na shughuli zake.

“Unajisikiaje mume wangu,” aliniuliza Khazija, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba naendelea vizuri. Tayari dripu ya maji ilikuwa imeisha, nesi akaja kunibadilishia na kuniwekea nyingine ambayo nayo iliendelea kuteremka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yangu.

“Aliishiwa maji kabisa nesi eeh! Kwani hii ni dripu ya ngapi?”

“Alikuwa na hali mbaya, hii dripu ya tano inakatika sasa ndiyo maana unaona anaweza hata kufumbua macho,” alisema, maneno yaliyopenya kwenye masikio yangu vizuri. Baadaye Khazija aliambiwa anatakiwa kutoka ili nipate muda wa kupumzika, kweli akatoka na kuniacha pale kitandani na muda mfupi baadaye nilipitiwa na usingizi mzito.

“Vipi unaendeleaje?” alisema daktari baada ya kuzinduka kutoka usingizini na kumkuta akiwa ananipima.

“Naendelea vizuri,” nilisema kwa sauti ya chini, akawa anatingisha kichwa kuonesha kwamba anaelewa nilichokuwa nakisema. Akaniuliza kama naweza kumsikia vizuri, nikamjibu kuwa namsikia vizuri.

“Una wake wangapi?”

“Mmoja tu!”

“Mara ya mwisho ulishirikiana kimapenzi na wanawake wangapi?”

“Mmoja tu,” nilisema huku nikigeuza kichwa changu pembeni kwa sababu sikufurahishwa na maswali yake, nikahisi sasa ananiingilia maisha yangu binafsi.

“Kwa uzoefu wangu, hali uliyokuwa nayo wakati unafikishwa hapa, huwa inawapata watu wenye wapenzi wengi na wanaoshiriki sana tendo la ndoa bila kupata muda wa kupumzika,” alisema huku akinitazama usoni.

Nilijikuta nikishikwa na aibu sana kwa sababu alichokuwa anakisema kilikuwa ni kweli kabisa.

Kwa siku chache zilizopita, nilikuwa nimeshirikiana kimwili sana, tena na wanawake tofauti tofauti, kuanzia Madam Bella, Salma sekretari wetu, mama mwenye nyumba, Khazija na Ruqaiya, achana na wale wa zamani wasio na idadi, hali ambayo ilinifanya nikose kabisa muda wa kupumzika.

“Jinsi kiuno chako kilivyokondeana inaonesha wazi kwamba huwa hakipati muda wa kupumzika, wewe ni kijana mwenzangu kwa hiyo lazima nikwambie ukweli, ipo siku utakuja kufia kifuani kwa kuendekeza haya mambo,” alisema daktari.

Ninavyojua mimi madaktari huwa wanafundishwa kuwa na lugha nzuri na za kutia matumaini kwa wagonjwa wao lakini huyu alikuwa akinikandia waziwazi.

“Mtu una mke mzuri kama huyu lakini inaonesha bado unaendekeza michepuko, tumekupima mkojo una karibu aina sita za UTI, tena sugu,” aliendelea kuninanga, akaniambia kwamba eti kiumri mimi ni kijana mdogo sana kuendekeza mambo kama hayo.

“Na bahati yako nimekupima ngoma huna, ukiendelea na mchezo huo muda si mrefu utakanyaga miwaya, we mtu gani unashiriki ngono mpaka unakaukiwa maji?”

“Dokta, mbona kama unakiuka miiko ya kazi yako? Kwa nini unanitolea maneno machafu kiasi hicho?”

“Wagonjwa wengine wa kujitakia kama wewe mimi huwa nawachana tu, hata ukiniona mnoko ndiyo nimekuchana, achana na ‘hizo mambo’ babu! Ungekuwa unaumwa Malaria au ugonjwa wowote wa kawaida ningekuonea huruma lakini siyo kwa hili tatizo lako la kujitakia,” alisema na kwa bahati nzuri, daktari mwingine ambaye kimamlaka alikuwa akionesha kama ana cheo kuliko yeye, aliingia.

Jinsi daktari huyo alivyo mnafiki, eti akabadilisha mada muda huohuo na kujifanya kama ananipa matumaini ya kupona kisha akawa ananikata jicho kama anayesema ‘ole wako unichongee’!

Kimsingi nilimchukia daktari huyo, unajua mara zote mtu anayesema ukweli hawezi kupendwa, niliona kama anaingilia mambo yasiyomhusu lakini kwa upande fulani kuna maneno aliyoyazungumza yalijirudia ndani ya kichwa changu na kunifanya nishindwe kuamini kama ni kweli au la.

“Na bahati yako nimekupima ngoma huna, ukiendelea na mchezo huo muda si mrefu utakanyaga miwaya, we mtu gani unashiriki ngono mpaka unakaukiwa maji?” maneno yaliyosemwa na daktari huyo bishoo ambaye alikuwa amevaa cheni shingoni yalijirudia kwenye kichwa changu.

Nikageuka na kumtazama, naye akanitazama kwa jicho la ukali, nikashusha pumzi ndefu na kuamua kuwa mpole.

“Kwa hiyo dokta, hebu sogea nikuulize vizuri,” nilisema kiungwana, basi akasita kidogo kisha akanisogelea huku akiwa amekunja uso wake.

“Kwa hiyo unasema kweli kwamba umenipima ngoma sina?”

“Demu wako ndiye aliyeniambia nikupime ngoma, na yeye amepima.”

“Majibu yakoje?”

“Huna, ila muda siyo mrefu utapata, we mtu gani unapenda ngono kuliko kula,” alisema na kuendelea ‘kunikazia’ kama mwanzo.

“Vipi mke wangu?”

“Hana, sema mwanangu demu wako kifaa kwelikweli,” alisema huku safari hii akianza kujichekesha. Nilishaelewa kwa nini anakuwa na chuki za kiasi hicho kwangu, unajua sisi wanaume, ukimuona mwenzako ana demu mkali au mke mzuri sana, basi hata kama hajakukosea kitu unaweza kujikuta tu ukianza kumchukia.

“Ninao wengi tu, tena wote wakali, nikupe pande mmoja nini?” nilimuuliza, akacheka sana na kunitania kwamba eti ndiyo maana nilikuwa nakaukiwa maji. Basi huo ulikuwa mwanzo wa urafiki kati yangu na daktari huyo ambaye naye alionesha kuwa ni mtu wa ‘totoz’ sana.

Hata hivyo, bado aliendelea kunisisitiza kwamba natakiwa kubadili mfumo wangu kwani nikiendelea kwa mtindo huo, kweli naweza kupata tatizo kubwa kiafya, ikiwa ni pamoja na kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Basi nilimuelewa kwa sababu safari hii alikuwa akizungumza nami kirafiki, kuna wakati mwingine pia alimshauri Khazija kwamba natakiwa kupata mapumziko ya kutosha siyo kila wakati nafanya tendo la ndoa tu.

“Huwa mwenyewe ndiyo anataka, sasa nashindwa kumkatalia,” alisema na kusababisha wote tucheke, akanigeukia.

Kiukweli moyoni nilifurahi sana kuambiwa kwamba licha ya sarakasi zote zile nilizokuwa nazifanya, sikuwa nimepata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na japokuwa mwenyewe aliniambia kwamba natakiwa kupima tena baada ya miezi mitatu ili niwe na uhakika, kwangu mimi nilishajihesabia kwamba nipo salama.

Nilimshukuru sana Khazija kwa uamuzi alioufanya wa kunipima bila mwenyewe kujua kwa sababu kiukweli sikuwa na ujasiri wa kwenda kupima na hata siku niliyojaribu, nilijikuta nikiishia kutoka nduki kutokana na hofu.

Basi niliendelea kupata tiba nyepesi za kurudisha nguvu mwilini kwani daktari alinieleza kwamba sikuwa naumwa isipokuwa mwili uliishiwa nguvu na maji kwa sababu ya kukosa muda wa kutosha wa kupumzika kwa sababu ya kuendekeza sanaa za kikubwa.

Baada ya kupumzishwa vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutundikiwa dripu, jioni niliruhusiwa kurudi nyumbani na daktari akanipa masharti kwamba natakiwa nisishiriki tendo mpaka baada ya siku saba, akanisisitiza kwamba natakiwa kula vizuri, kupata muda wa kupumzika na kufanya mazoezi mepesi angalau mara tatu kwa wiki.

Nilimshukuru sana, Khazija akalipa gharama za matibabu na tukatoka mpaka nje ambako tuliingia kwenye Bajaj na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Angalau sasa mwili wangu ulikuwa na nguvu japokuwa nilikuwa nimepungua uzito kwa kiasi kikubwa mpaka mwenyewe nikawa najishangaa.

Tulipofika nyumbani, Khazija alinishauri nifikie kwake ili aniandalie msosi, wazo ambalo nililiona kuwa la busara. Kweli dada wa watu alijitahidi sana kunihudumia, kwanza alinipelekea maji bafuni ambako baada ya kuoga kidogo nilijisikia ahueni.

Niliporudi ndani tayari alikuwa ameniandalia supu, baadaye kidogo akaandaa chakula kizuri na baada ya kula, hatimaye tulilala. Kwa mara ya kwanza tuliweza kulala mpaka asubuhi bila kufanya chochote kulingana na masharti ya daktari.

Kesho yake pia sikuweza kwenda kazini kwani bado sikuwa vizuri kiafya, kwa kuwa tayari walikuwa wanajua kwamba naumwa, hakukuwa na tatizo. Kutwa nzima nilishinda ndani na Khazija akinihudumia kwa kila kitu kama mtoto mdogo.

Siku iliyofuatia niliweza kujikongoja na kwenda kazini ingawa nililazimika kuvaa nguo kubwakubwa ili kuficha wembamba wa ghafla uliokuwa umenikumba.

Kama tulivyokuwa tumekubaliana na Khazija usiku uliopita, nilikuwa na kibarua kigumu cha kuwaeleza wanawake wangu wote kwamba nimepata mchumba na najiandaa kuoa kwa hiyo tupunguze mazoea.

Khazija alikuwa amenipa ‘option’ hiyo kwa sababu ilibidi niwe mkweli kwake, nikamwambia kwamba kabla ya kukutana naye nilikuwa na wanawake wengi ambao kila mmoja aliniganda kama ruba na sijui namna ya kuwaacha.

Wa kwanza kukutana naye alikuwa ni Salma, mfanyakazi mwenzangu ambaye yeye alikuwa kitengo cha reception, aliponiona tu aliinuka kwenye kiti chake na kuja kunikumbatia kwa nguvu, akawa ananipa pole kwa kuugua.

“Kweli umepatikana baby wangu, cheki ulivyokonda ndani ya siku mbili tu,” alisema Salma huku akitabasamu kwa bashasha, akaona kama haitoshi, anibusu mdomoni, akawa ananiambia jinsi alivyonimisi.

Nilijitahidi sana kuukwepa ukaribu wake lakini haikuwa rahisi, akawa anaendelea kunipigisha stori za hapa na pale huku akiwa bado amening’ang’ania mwilini. Ilibidi nimtoke kijanja na kwenda ofisini kwangu. Kazi zote zilikuwa zimesimama na kubaki vilevile kama nilivyoziacha, waliosema penzi kitovu cha uzembe hawakukosea.

Mambo ya wanawake yalikuwa yamesababisha nishindwe kabisa kufanya kazi kama ilivyokuwa awali na kwa picha ile niliyoiona, nilijua kabisa kwamba kama nitashindwa kujirekebisha, hata kazi yenyewe naweza kuipoteza.

Moyoni nilijihisi kuwa na hatia kwa sababu sikutimiza wajibu wangu ipasavyo na kwa namna moja au nyingine, nilikuwa naiibia kampuni kwa kuwa nilikuwa nalipwa mshahara ambao sikuufanyia kazi. Kwa upande mwingine, nilimtupia lawama bosi, Madam Bella kwani naye pia alikuwa chanzo cha mimi kuzembea baada ya kuanza kuingiza masuala ya mapenzi.

Nikiwa nawaza nianze na kazi ipi, simu ya mezani iliita, nilipopokea alikuwa ni Salma, mdada wa mapokezi, akaniambia kwamba bosi amesema niende ofisini kwake, nikajua picha limeanza upya. Nilitoka na kwenda mpaka ofisini kwa bosi, nilipoingia tu akainuka pale alipokuwa amekaa na kunikimbilia, akanikumbatia kwa nguvu huku akionesha kuguswa sana na hali yangu maana nilikuwa nimepungua ghafla.

“Pole sana mume wangu,” aliniambia huku akinibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, akaniambia kama bado nahisi sijapata nguvu, kwa nini nisipumzike tu nyumbani?

“Mh! Na kazi zangu atafanya nani bosi? Bora nijikaze tu, nimeshapona bado mwili kukaa sawa tu,” nilimwambia, akaniambia anataka nipone haraka kwani amemisi sana ‘mambo yetu’, tukacheka na kugongesheana mikono, akanikumbatia tena na kusababisha manukato mazuri aliyojipulizia yapenye kwenye pua zangu na kunipa burudani ya aina yake.

Kitu kimoja nilichokuwa nampendea Madam Bella, alikuwa anajipenda sana, muda wote ukimuona yuko ‘smart’, ananukia vizuri hadi raha. Wakati yeye akifurahia kuniona tena, mimi nilikuwa na mtihani mkubwa wa namna ya kumfikishia ujumbe kwa sababu kiukweli alionesha kunipenda mno mpaka nikawa najisikia vibaya.

INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.