Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Ishirini na mbili (22)
Hata hivyo, jambo lisilo la kawaida lilitokea. Mkuu wa kaya hakutaka kabisa kuonesha ushirikiano, hata sijui alikuwa amekumbwa na balaa gani kwani muda wote alinywea na licha ya jitihada zilizofanywa na Ruqaiya za kumrudisha mchezoni, aligoma kabisa.
“Una nini wewe?”
“Hata sijui, mimi mwenyewe nashangaa.”
“Siyo kawaida yako, au huwa unatokewa na hali kama hii?”
“Hapana! Mimi mwenyewe najishangaa.”
“Ulikuwa na mwanamke humu ndani si ndiyo?”
“Mimi?”
“Ndiyo wewe kwani naongea na nani?”
“Hapana Ruqaiya, siyo kweli! Unanihisi vibaya tu jamani.”
“Sasa kwa nini imekuwa hivi? Unafikiri itakuwaje wakati hali yangu ndiyo kama unavyoiona na nimehangaika kutwa nzima ya leo kukutafuta ili uutibu moyo wangu, kwa nini lakini unanifanyia hivi,” alisema Ruqaiya huku machozi yakianza kumlengalenga.
“Ukinilaumu unakosea Ruqaiya!”
“Nakosea? Nakosea nini? Kama hukuwa na mwanamke aliyemaliza kila kitu humu ndani kwa nini imekuwa hivi?” Ruqaiya alicharuka. Tangu nimfahamu sijawahi kusikia akizungumza kwa sauti ya ukali kiasi hiki, nikawa na kazi ya kumbembeleza.
Licha ya kujitahidi kumbembeleza kwa muda mrefu hakutaka kusikia la muadhini wala la mchota maji, alikuwa akilia kama mtu aliyepokea taarifa za msiba huku mkono wake mmoja ukiwa kwenye chungu cha asali!
Nilijisikia vibaya sana kwa kushindwa kufanya kile kilichomfanya awali akanipenda na kuniheshimu kiasi cha kufikia hatua ya kuacha kila kitu chake na kufunga safari kunifuata.
Mara nilipata wazo la kutoka kwenda kwa Mangi ‘kubusti’, nikajishangaa kwa nini sikupata wazo hilo haraka?
“Nisubiri naenda dukani mara moja,” nilimwambia lakini hakunijibu chochote, harakaharaka nikavaa na kutoka, ili kuzuia Khazija asije akaingia na kuharibu mambo, nilifunga mlango kwa nje na funguo, nikanyata kimyakimya na wakati nikimalizikia kutoka getini, nilisikia ‘msonyo’ mkali kutokea ndani, bila hata kuuliza niligundua kwamba ni mama mwenye nyumba.
Tabia aliyokuwa ameamua kuianzisha mama mwenye nyumba, ya kunitolea misonyo kila anaponiona na mwanamke, ilinifanya nijisikie vibaya sana ndani ya moyo wangu. Ni kweli nilikuwa nimeangukia naye dhambini mara kadhaa lakini ukweli ambao hata yeye alikuwa anaujua ni kwamba sikuwa nampenda.
Ilitokea tu kwamba tumeangukia dhambini lakini si kweli kwamba nilikuwa na mapenzi naye, na hata kama alikiri kwamba nimemfanya ajisikie tofauti kabisa katika uwanja wa huba, hicho hakikuwa kigezo cha yeye kuanza kuingilia maisha yangu na kuniamulia nini cha kufanya.
“Mbona yeye analala na mume wake lakini mimi simsemeshi chochote?” nilijisemea wakati nikiongeza mwendo kuelekea dukani kwa Mangi.
“Mbona siku hizi unabusti sana babaake? Zina madhara hizo, siku nyingine utakuwa huwezi kabisa,” Mangu muuza duka aliniambia wakati akiniohudumia lakini sikumjali. Najua utakuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nilikuwa nabusti vipi, potezea nitakueleza siku nyingine.
Nilijibusti harakaharaka, nikanunua na ‘big g’ na kuchangamsha mdomo, harakaharaka nilimlipa na kuondoka kurudi kwangu, huku mkononi nikiwa nimenunua vocha na juisi ili hata akiniuliza nilifuata nini niwe na majibu.
Nilifanikiwa kuingia ndani kimyakimya bila mtu yeyote kushtukia, nikaufunga mlango kwa ndani huku nikijitahidi sana kuvuta pumzi ndefu na kuzitoa ili kutuliza akili maana kama akili haijatulia hata ukijibusti ni kazi bure.
“Nimekuletea juisi.”
“Aliyekwambia nimefuata juisi kwako ni nani?”
“Jamani Ruqaiya mbona unakuwa mkali kiasi hicho?”
“Hiki ni nini?” alisema Ruqaiya huku akinionesha kitu ambacho kilinshtua mno moyo wangu.
“Umeipata wapi kwani?”
“Nijibu swali langu,” alisema huku safari hii akiinuka na kukaa kitako pale kitandani. Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio nikiwa hata sijui nitamjibu nini. Kumbe mara ya mwisho Khazija alipoingia mle ndani tukavurugana kisawasawa, aliacha ‘kufuli’ lake pale chini bila mimi kujua.
“Aah, unajua jana nilifua nguo, sasa wakati wa kuanua nilichelewa nikaanua usiku na hapa kuna mabinti wana kawaida ya kuanika nguo zao hadharani, inawezekana nilijichanganya lakini nakuhakikishia hakuna mtu aliyeingia humu ndani,” kidume nilimwaga uongo wenye kasi ya 4G, hata sijui nilipata wapi akili hiyo lakini huwezi kuamini, Ruqaiya aliniamini kabisa.
“Kwani hawajafundwa mpaka waanike nguo za siri hadharani, wasichana wengine sijui wakoje! Kaitupe nje,” alisema huku akiisukumia pembeni na mguu wake, nikaona hapohapo ndiyo muda wa kujaribu tena bahati yangu.
Nilifanya kama kumshtua kidogo hivi kwenye mbavu zake, basi akaruka mzimamzima utafikiri amekanyaga moto na kutoa kasauti fulani hivi ‘amaizing’, nikajikuta nimesisima mno.
“Unanitesa bure wakati unajua huwezi kuninanii!”
“Kufanyeje?” nilimuuliza huku nikiisogeza sura yangu karibu na yake. Mkono mmoja nikalishika shavu lake la kushoto na kumsogeza karibu, nikambusu, naye akafanya hivyohivyo, nikafanya hivyo tena huku roho yangu ikipata burudani ya aina yake kutokana na jinsi alivyokuwa mzuri, muda mfupi baadaye tukagusanisha ndimi zetu na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa tofauti kabisa.
Hatua zile zilifanikisha azma yangu kwani gari liliwaka ‘fasta’, alipopeleka mkono na kukutana na kitu kigumu, nilimuona akinitazama kwa kushtuka kisha akawa anayarembua macho yake huku tabasamu fulani hivi la aina yake likiupamba uso wake na kumfanya azidi kuwa mrembo.
Hakuwa na muda wa kusubiri, alijiweka katika mkao wa kula, akanivuta mzima mzima na kumuelekeza ‘mkuu wa kaya’ kwenye sehemu anayotakiwa kuwepo kwa wakati huo. Kwa jinsi alivyokuwa amenibana, ungeweza kudhani tuna ugomvi au anahisi naweza kuchoropoka na kukimbia, moyoni nikawa najiambia kwamba ‘utaomba po mwenyewe’.
Basi mtanange wa kukata na mundu uliendelea, utafikiri mechi ya fainali ya UEFA kati ya Ral Madrid na Liverpool ilivyokuwa kali, ikawa ni piga nikupige! Niliamua kufanya kweli kwa sababu lawama alizokuwa amenitolea zilikuwa kali sana, kazi yangu ikawa ni kufuta makosa.
Nilimvuruga kwelikweli, ikafika mahali akaniachia mwenyewe huku akitoa kiguno ya hapa napale ambayo ilizidi kunihamasisha, nikaendelea kuonesha umahiri wa kucheza na mpira, mara nipige danadana, mara nimpige tobo, mara nimpige darizi, basi ilikuwa burudani kwelikweli.
“Kwani tuna ugomvi baba?”
“Hapana mama!”
“Mbona kama unanikomoa sasa?”
“Mimi? Mbona unanisingizia mama?” nilisema huku nikitabasamu, nikaendelea kufanya mambo na muda mfupi baadaye, Ruqaiya alijifunga bao moja matata sana, bila kutegemea akajikuta akishangilia kwa sauti ya juu ambayo bila hata kuuliza nilijua lazima itafika kwa Khazija.
Sikujali sana, nikawa naendelea kulisakata kabumbu huku nikilishambulia sana lango lake na muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimewamaliza mabeki wake wote, nikabaki mimi na golikipa tu, wakati najiandaa kupiga shuti kali, mara nilisikia mlango ukigongwa.
“Ngo! Ngo! Ngo!”
Akili ilihama kutoka mchezoni na kwenda mlangoni, nikawa najiuliza ni nani anayeweza kuwa anagonga kwa muda huo? Hata hivyo, huwezi kuamini nilipuuzia na kurudisha akili mchezoni, nikapiga shuti kwa nguvu na mpira ukaenda moja kwa moja nyavuni.
Ruqaiya alinikamata kwa nguvu sana huku macho yake akiwa ameyafumba kisha taratibu akaanza kuniachia, nikadondokea upande wa pili huku miguu ikitetemeka utafikiri nimetoka kufanyishwa mazoezi makali ya kutingisha misuli gym.
Bado mlango uliendelea kugongwa lakini sikujali, nikawa nimejilaza huku nikipumua utafikiri nimetoka kukimbia mbio za marathon, kijasho chembamba kikinitoka.
“Mume wangu!” Ruqaiya aliniita kwa sauti ya chini. Kwa jinsi alivyoniita kimahaba, nilijikuta nikisisimka sana, nikamsogelea na kumtazama machoni, naye akawa ananitazama kwa macho yake ya kurembua.
“Nani tena huyo anagonga mlango?”
“Watakuwa ni hao watoto wa mwenye nyumba, achana naye mke wangu,” nilisema na kumbusu kwenye paji la uso, akanikumbatia tena kisha tukagusanisha ndimi zetu.
“Yaani ningekuwa sijaolewa, lazima wewe ndiyo ungekuwa mume wangu, unanifanya nijisikie kama mwanamke niliyekamilika, ahsante sana baba,” aliniambia kwa sauti ya kunong’ona iliyopenya kwenye masikio yangu na kunifanya nijihisi kama nipo kwenye ulimwengu wa tofauti kabisa.
Unajua miongoni mwa ‘maradhi’ waliyonayo wanaume wengi, ni kupenda kusifiwa baada ya kumaliza kulisakata kabumbu. Na baadhi ya wanawake nao ni kama wameshajua huu udhaifu, akitaka kukuchuna hata kama umecheza chini ya kiwango atakupamba kwa sifa kedekede ilimradi apate anachokitaka.
Hata hivyo, mimi nilikuwa najua kwamba Ruqaiya anachokisema kinatoka ndani ya moyo wake kwa sababu ni kweli nilikuwa nimemuweza na ukitaka kujua kama kweli umemuweza mwenzi wako, zipo dalili za waziwazi ambazo huwa hazijifichi anapofika pale anapopataka muwapo faragha.
Unajua kukua kwa sayansi na teknolojia, kumewafanya wanawake kujifunza uongo mwingi sana wawapo faragha na wanaume wao. Kuna wakati mwingine anaweza kukuektia kama ameiona theluji ya Mlima Kilimanjaro kumbe hakuna chochote, anataka kukufariji tu lakini moyoni anakudharau kwa jinsi ulivyoshindwa kuonesha ukakamavu wa kumtoa chozi la utamu.
“Unasema kweli mke wangu?”
“Kweli baba, unajua nilishakwambia kuanzia mwanzo mimi kuwa na wewe siyo kwamba nina tabia ya kutokatoka hovyo na wanaume, mume wangu ananipa kila kitu ninachokihitaji, wewe ni shahidi kwamba sina shida ndogondogo lakini kuna kitu kikubwa sana nakikosa kwa mume wangu,” aliniambia kwa sauti ya chini.
Akanibusu tena na kuendelea kunieleza kile alichonieleza siku chache zilizopita kwamba mumewe alikuwa na tatizo la kushindwa kumfanya afike mwisho wa safari yake wawapo faragha, jambo ambalo limemtesa kwa kipindi kirefu mpaka alipokutana na mimi.
“Ilifika mahali nikawa nachukia hata kukutana naye maana najua tu kwamba hata ajitahidi vipi, ataniacha mwenzake kwenye hali mbaya, lakini siyo wewe,” alisema huku akinipigapiga kifuani, nikafurahi sana.
“Lakini nakuomba sana, huo ‘ukivuruge’ wako hebu achana nao, nitakupa kila utakachokihitaji. Unajua mimi ni mwanamke mwenye heshima zangu sasa kushea mapenzi na visichana viruka njia ni jambo ambalo siwezi kabisa kulivumilia, naomba unielewe sana kwenye hili suala,” alisema Ruqaiya, nikajifanya mtiifu sana na kuitikia kila alichokuwa ananiambia.
“Najua lazima utakuwa na visichana vyako ulivyotoka navyo huko nyuma, nakupa muda wa kuweka mambo yako sawa, ukiwa mwaminifu kwangu utafaidi sana lakini usiponiheshimu basi...” alisema Ruqaiya huku akionesha kumaanisha kwelikweli kile alichokisema.
“Usijali mama, mbona nimeshabadilika sana, unajua tangu nilipokutana na wewe, umenibadilisha kwa vitu vingi sana, inawezekana wewe mwenyewe hujui lakini huo ndiyo ukweli,” nilizidi kumpiga fiksi.
Yule mtu aliyekuwa akigonga mlango hakuendelea tena kugonga lakini kwa ugongaji ule, nilijua lazima atakuwa ni Khazija, kichwani nikawa napanga mistari ya namna ya kumdanganya.
Unajua watu wengi hawajui lakini ukweli ni kwamba mwanaume au mwanamke msaliti, hawezi kuwa na amani ndani ya moyo wake hata kidogo. Yaani muda wote anakuwa anafikiria jinsi ya kudanganya ili kuweka mambo sawa au kufikiria nini kitatokea endapo usaliti wake utagundulika.
Ndiyo maana mtu msaliti, kila anapokaa anakuwa mtu wa machale tu, hataki kukaa mbali na simu yake na hata akiiacha mbali, basi ujue imewekwa password kila sehemu na imetolewa mlio na kugeuziwa chini ili hata mtu akipiga asijue mtu yeyote.
Ukiona uko na mwenzi wako lakini simu ameweka silence halafu ameigeuzia kioo chini, na muda wote anaitazamatazama jua kuna namna hapo, hiyo ni tabia ya watu wasio waaminifu.
“Mbona kama unawaza, unafikiria nini?” Ruqaiya alinizindua kutoa kwenye lindi la mawazo, nikajifanya kujichekeshachekesha pale lakini ukweli ni kwamba nilikuwa naifikiria sana kauli aliyoitoa Khazija kwa sababu naye alinitishia kwamba eti kama sitabadilika kitabia na kutulia, ataenda kuniroga ili jogoo wangu asiwe anapanda mtungi ninapofikiria kumsaliti.
“Potelea mbali,” nilijiambia ndani ya moyo wangu kwa sababu ni kweli Khazija alikuwa ananipatia sana tuwapo faragha lakini kuwa na watu kama Ruqaiya kwenye maisha yangu, lilikuwa ni jambo muhimu sana.
“Nakuahidi nitakuwa mwaminifu sana kwako na nitajitahidi kutunza siri ili nisikuharibie ndoa yako,” nilimwambia, basi akafurahi sana na kunikumbatia huku akinimwagia mvua ya mabusu.
Haukupita muda tukarudi tena uwanjani, safari hii aliniomba niende naye ‘mdogo-mdogo’ kwani hakuwa amezoea ‘masebene’ kama yule msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kuimba ‘sijazoea masebene miee’, hata sijui jina lake anaitwa nani.
Wakati tukiendelea kulisakata kabumbu katika kipindi cha pili, kuna wakati mwenzangu uzalendo ulikuwa ukimshinda na kumfanya atoe miguno ya hapa na pale ambayo ilipaa na kutoka mpaka nje.
Nikaanza kusikia misonyo ya mama mwenye nyumba ikiambatana na vicheko vya kebehi, mimi nikawa sijali, nikajifanya kama sisikii chochote. Mtanange wa nguvu uliendelea na baadaye, Ruqaiya alizifumania nyavu na muda mfupi na mimi nikazifumania, ikawa ngoma droo.
Kutokana na uchovu niliokuwa nao, nilijikuta nikipitiwa na usingizi mzito, Ruqaiya naye akalala fofofo. Nilipokuja kuzinduka baadaye, tayari ilikuwa ni usiku, nikamuamsha Ruqaiya ambaye alipogundua kwamba tayari ni usiku alishtuka kuliko kawaida.
“Nisindikize.”
“Si ukaoge kwanza?”
“Hapana, nimechelewa sana, daah! Kwa nini umeniacha nimelala hivi?” Ruqaiya alianza kunilaumu, ikabidi nimtulize kwanza mpaka alipotulia. Sikuona kama ni busara kwa yeye kuondoka vilevile alivyokuwa, kwa bahati nzuri alikubaliana na mimi kwenda kuoga.
Nilitembea kwa kunyata mpaka mlangoni, nikafunua pazia na kuchungulia nje kupitia kitundu cha funguo na nilipojiridhisha kwamba hakuna mtu yeyote pale nje, nilifungua mlango taratibu sana.
Nikaenda kumchukua Ruqaiya na kwa sababu zangu maalum, niliamua tuongozane mpaka bafuni. Yeye aliamini kwamba mahaba mazito ndiyo yanayonisukuma kufanya hivyo kumbe mimi nilikuwa na sababu zangu nyuma ya pazia. Basi tulioga pamoja huku nikiendelea ‘kumuektia’, akaniambia mume wake hajawahi kwenda naye bafuni kuoga hata mara moja.
Tulirudi ndani na ile tunaingia tu, nilisikia mlango wa chumba cha Khazija ukifunguliwa, mapigo ya moyo yakanilipuka na kuanza kudunda kwa nguvu, nikawa sijui nini kitakachotokea.
Ni kama Khazija alikuwa anajua kila kinachoendelea na sasa alitaka kupata ushahidi tu maana alipofungua mlango wake, wala hakujishughulisha kuja kwangu kama nilivyokuwa nimefikiria bali alitoka na kukaa mlangoni huku macho yote yakiwa kule kwenye mlango wangu.
“Aah, potelea mbali, liwalo na liwe!” nilisema huku na mimi nikianza kujiandaa kwa ajili ya kumsindikiza Ruqaiya. Baada ya kumaliza kujiandaa, na yeye akiwa ameshamaliza kujiandaa, nilimtanguliza yeye nje.
Bila hata kujua kwamba nje kulikuwa na hali ya hatari, Ruqaiya alimsalimu Khazija, naye akaitikia kwa uchangamfu kama hakuna kilichotokea. Na mimi nilitoka na kufunga mlango kwa funguo kisha tukawa tunatoka na Ruqaiya.
Kumbe si Ruqaiya tu aliyekuwa ametoka nje, hata mama mwenye nyumba naye alikuwa ametoka nje na baada ya kuhisi kama sijamuona, alijikoholesha kwa makusudi na kuanza kuimba nyimbo za taarabu zenye mafumbo.
“Huku kwenu Uswahilini kwelikweli, naona hata watu wanaoishi huku wote akili zao zinafanana,” alisema Ruqaiya wakati tukitoka, nikamuuliza kwa nini?
“Wewe si umeona yule sijui ndiyo mama mwenye nyumba wako anavyoimba taarabu kwa mafumbo? Hajui kama mafumbo na ‘mastashtiti’ hapa yamelala? Halafu kile kisichana nacho kwa nini kimekaa pale nje kwa makusudi?”
“Inabidi uyazoee tu mazingira ya huku mama, hakuna namna.”
“Akuu, mi siwezi kuzoea Uswahili wa kiasi hiki! Kwanza unaonaje nikikutafutia nyumba sehemu nyingine tofauti na Tandale? Mi nataka mahali ambapo nitakuwa huru,” alisema Ruqaiya, nikacheka sana.
Nilicheka kwa jinsi alivyokuwa amelichukulia suala hilo lakini kubwa nilicheka kwa furaha baada ya kuona kwamba nimefanikiwa kumtoa salama maana sasa tulikuwa tukikaribia kufika pale alipokuwa amepaki gari lake.
“Sasa mimi naongea na wewe mambo ya maana halafu unanicheka, kwa nini?” alisema Ruqaiya huku akinikumbatia bila hata woga. Unajua mapenzi yana sifa moja kubwa ambayo inawezekana wengi hawaijui.
Mnaweza kuwa na uhusiano wa kisiri wa mapenzi lakini yatakapokolea tu, mtajikuta mkifanya mambo ambayo kwa watu wanaoelewa, wanaweza kabisa kugundua kwamba mpo kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Ruqaiya kwa sababu nakumbuka siku ya kwanza hata kumgusa mkono wake tu alikuwa hataki mpaka tuwe sehemu ambayo hakuna mtu mwingine anayeweza kutuona lakini ajabu ni kwamba siku hiyo yeye ndiyo alikuwa akinikumbatia mara kwa mara.
Yaani kama angetokea mtu anayemfahamu, halafu akamuona alivyokuwa akinifanyia, ni dhahiri taarifa zingeenda moja kwa moja kwa mumewe.
“Huogopi kunifanya hivyo hadharani?” nilimuuliza.
“Niogope nini?”
“Wapambe wakimwambia mumeo je?”
“Hata akiambiwa hana cha kufanya, kwa jinsi anavyonipenda nitamuomba msamaha na yataisha. Hata akiniacha wewe si utanioa?” alisema huku akinikumbatia tena na kunibusu, tukaishia kucheka.
“Inabidi twende kwa yule rafiki yako Ras kumshukuru maana bila yeye sijui kama ningekupata leo.”
“Aah! Usijali, nitaenda kumshukuru mimi, twende nikusindikize uende zako maana huku kwetu siyo salama kabisa, wanaweza kukuvua hizo dhahabu zako,” nilimwambia, akacheka sana. Tayari tulishafika pale alipokuwa amepaki gari lake, tukaingia.
“Yaani japokuwa nimechelewa kiasi hiki lakini eti huwezi kuamini bado natamani kuendelea kukaa na wewe,” alisema Ruqaiya, wote wawili tukacheka sana na tukaishia kukumbatiana kimahaba.
“Nakupenda sana baby! Nakuomba zingatia nilichokwambia, nataka utulie na mimi tu nitakupa chochote ukitakacho,” alisema kwa sauti ya kimahaba huku akiwa amenikumbatia, nikatingisha kichwa kama ishara ya kumkubalia, akanibusu kwenye mdomo wangu na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumegusanisha ndimi zetu.
Ilibidi mimi ndiyo nimhimize awahi kuondoka maana muda ulikuwa ukizidi kuyoyoma, nikafungua mlango wa gari ili nishuke.
“Nilikuletea zawadi yako, chukua,” alisema huku akitoa bahasha kwenye ‘dash-board’ ya gari na kunikabidhi. Ilikuwa imetuna na kwa haraka sikujua ndani yake ina nini, nikamshukuru kisha nikamsaidia kumuelekeza namna ya kutoa lile gari mpaka alipoingia barabarani, akanipigia honi ya kuniaga na kuondoka zake.
Niliingiza mkono mfukoni na kuitoa ile bahasha, sikuamini nilichokutana nacho. Ilikuwa imejaa noti mpya za shilingi elfu kumikumi, nikajikuta nikishindwa kujizuia, nikapiga kelele za kufurahia kisha nikaisokomeza mfukoni na kuanza kutembea harakaharaka kwenda kwa Ras.
Nilitaka nikamshukuru kwa kumleta Ruqaiya kwa sababu kama asingemleta, nisingepata fedha nyingi kiasi hicho na mahaba juu.
“Dah! Umempata wapi mwanamke mzuri kiasi kile na unamfanyiaga nini maana inaonesha anakupenda kwelikweli, mpaka alikuwa analia machozi hapa, waulize washkaji.”
“Kweli mwanangu, amekaa sana hapa anakusikilizia mpaka akawa analia! Ukimcheki mtu mwenyewe daah! Ebwana unatembea na hirizi nini wewe?”
“Hamna washkaji, kawaida tu,” nilisema huku nikivunga. Sikutaka kabisa kutoa siri ya kambi kwa washkaji, isitoshe hata akili yangu haikuwa imetulia kwa sababu mfukoni nilikuwa na fedha nyingi sana.
Basi nilizugazuga pale, nikatoa shilingi elfu kumi na kumshikisha Ras bila mtu yeyote kuona kisha nikaaga na kuondoka, huku nyuma nikaacha gumzo kubwa kwa sababu kila mtu alikuwa anataka kujua nimefanya nini mpaka mwanamke mrembo kama yule anizimikie kiasi cha kumwaga machozi hadharani.
Wakati natembea nilikuwa najiuliza maswali mengi sana ndani ya kichwa changu kwa sababu hata mimi mahaba aliyokuwa akinionesha Ruqaiya yalinifanya nikose msimamo na nishindwe kuelewa nini cha kufanya.
Ni kweli nilikuwa nimeshaanza kumpenda Khazija lakini mahaba ya nguvu aliyonipa Ruqaiya, ukichanganya na zawadi zake, nilijikuta nikijiuliza tena kama kweli nataka kuingia kwenye uhusiano ‘siriasi’ na Khazija au la!
“Mwana FA unaoa lini... bado niponipo kwanza! Bado niponipo mwana...” nilijikuta nikiimba huku nikipiga na mbinja. Nilikuwa najiimbia tu kwa sababu napenda sana muziki wa Bongo Fleva lakini kumbe kwa wengine, walikuwa wakinitafsiri tofauti kabisa.
Walioniona nikipita na Ruqaiya walidhani eti naimba hivyo kama ishara ya kujisifia kwa jinsi ninavyoweza ‘kung’oa’ wanawake wazuri wakati mimi mwenyewe sina mbele wala nyuma.
“Bado niponipo sa...” nilishindwa kumalizia kuimba baada ya kugongana uso kwa uso na Khazija. Kumbe kwa muda wote huo alikuwa amejibanza nje akinisubiri na inavyoonesha aliuwa akinifuatilia hata wakati namsindikiza Ruqaiya.
“Yule ni nani?” aliniuliza kwa ukali huku sauti yake ikitoka kwa kutetemeka.
“Khazija... kwa nini tusiende kuzungumzia ndani?”
“Nataka unipe majibu hapahapa, yule ni nani?” alisema Khazija huku akipandisha sauti kiasi cha kuwashtua watu waliokuwa pale dukani kwa Mangi, nikawaona wote wakigeuka na kututazama.
“Jamani Khazija, mambo gani tena hayo unayotaka kunifanyia mke wa...” hata sikumalizia kauli yangu, nikashtukia kofi kali likitua kwenye paji langu la uso, Khazija akanivaa mzimamzima na kunidondosha chini na katika kile ambacho sikukitegemea, nilishangaa akichomoa kisu na kukishika kwa mkono wake wa kulia huku mkono wa kushoto akiwa amenikaba, akawa anataka kukizamisha kifuani kwangu.
“Leo nakuua, shetani wewe. Hauwezi kucheza na moyo wangu halafu nikuache,” alisema huku akitetemeka kwa jazba.
“Sikia Khazija, nakuomba mama tukayaongee ndani.”
“Ukaongee na mimi nini? Wewe si unajifanya kidume sana, sasa leo ndiyo utanijua,” alisema Khazija huku akiwaka kama moto wa gesi, nikajua nisipofanya jambo anaweza kweli kuniua.
Tayari watu walishaanza kujaa, kama unavyojua tena mitaa ya uswahilini kwetu hata tukio litokee saa nane za usiku watajaa watu mpaka utashangaa walikotokea.
Basi niliamua kutumia uanaume wangu, nikapitisha mguu kutokea mgongoni kwa Khazija na kwenda kuubana ule mkono aliokuwa ameshika kisu, kufumba na kufumbua nikamsukuma kwa kutumia ule mguu, akadondokea upande wa pili.
Kwa kasi kubwa niliinuka na kutimua mbio kukimbilia ndani, kwa bahati nzuri geti lilikuwa wazi, nikaingia na kwenda ndani kwangu moja kwa moja, nikajifungia mlango kwa ndani. Kelele nilizoendelea kuzisikia nje zilikuwa kubwa sana, kuonesha kwamba Khazija alikuwa ananifuatilia huku wapambe wakiwa wanashangilia.
Tangu nimfahamu Khazija sikuwahi kudhani kama anaweza kuwa na akili mbovu kiasi hicho, ni kweli nilikuwa nimemkosea lakini sasa ndiyo anishikie kisu? Ukisalitiwa basi ndiyo umuue aliyekusaliti? Nilishindwa kupata majibu, moyoni nikawa naijutia nafsi yangu kwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Khazija.
Unajua kwa kipindi kirefu nilikuwa nikishangaa sana kusikia stori kwamba sijui mwanamke fulani amemuua mumewe baada ya kugundua kwamba anamsaliti, mara sijui mwanaume amekatwa nyeti na mkewe kwenye fumanizi na nyingine kama hizo. Nilikuwa naamini kwamba kwa jinsi wanawake walivyoumbwa, hawawezi kuwa na roho mbaya kiasi hicho lakini sasa yalikuwa yamenifika kooni.
“Nakwambia toka nje kama wewe kidume kweli,” alisema Khazija huku akigongagonga mlango wangu kwa nguvu. Yaani kama isingekuwa kufunga kabisa mpaka geti la chuma kwa funguo, huenda angeniingilia mpaka ndani.
Kwa bahati nzuri, mama mwenye nyumba alitoka na kitu cha kwanza alichokifanya, ilikuwa ni kumtaka Khazija aache kumjazia watu kwenye nyumba yake. Harakaharaka akawatoa wapambe waliokuwa wakishadadia wakitaka kujua nini kinachoenda kutokea na kufunga mlango mkubwa wa geti.
“Wewe, unamshikia nani kisu? Kumbe tunaishi na mwendawazimu humu ndani? Mnataka kuuana hapa kwangu mniletee kesi si ndiyo? Kesho unahama,” alisema mama mwenye nyumba kwa hasira, Khazija akakitupa kile kisu na kuanza kulia kwa sauti ya juu.
Nilijikausha ndani kama siyo mimi, akalia sana pale nje na baadaye nilimsikia akiinuka na kwenda chumbani kwake, nikawa na wasiwasi kwamba huenda baada ya kunikosa, anaweza hata kujiua.
Sikuwahi kukutana na mwanamke mwenye hasira kali kama Khazija, moyoni niliapa kama sakata hilo litapita salama basi huo ndiyo mwanzo na mwisho wa kuwa naye karibu kwa sababu kweli siku anaweza kuja kuniua.
“Hebu fungua mlango,” sauti ya mama mwenye nyumba ilisikika, nikashtuka maana bado nilikuwa nimekaa kwenye kochi kama sanamu. Nilifungua mlango wa ndani lakini geti sikufungua, tukawa tunatazamana na mama mwenye nyumba huku nikiwa na hofu kubwa.
“Unaona ujinga wako unavyotaka kusababisha maafa hapa nyumbani kwangu? Hivi wewe una nini? Huwezi kabisa kutulia na mwanamke mmoja, au umerogwa mwenzetu?” aliniuliza mama mwenye nyumba, nikakosa cha kujibu zaidi ya kujiinamia chini.
“Una bahati mume wangu amesafiri jioni hii, angekuwepo leo wote mngeenda kulala ndani, wewe na huyo changudoa wako! Na nimeshamwambia atafute nyumba ya kuishi, siyo hapa kwangu, siwezi kuishi na vichaa mimi. Na wewe...” alisema huku akinitazama usoni, nikajua tu kauli inayofuata ni kuniambia ‘uhame hapa kwangu, sikutaki’.
“Lakini mimi sina kosa mama, yeye ndiye aliyenishikia kisu,” nilimkatisha, akanitazama kisha akameza funda la mate, akageuka huku na kule kuangalia kama hakuna mtu aliyekuwa akitutazama.
“Fungua mlango nakuja tuongee vizuri,” alisema kwa sauti ya chini, akageuka na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea ndani kwake.
“Hapana mama naomba tuongee kesho, sipo vizuri kabisa kwa sasa,” nilisema, akageuka na kunitazama kwa jicho la ukali kama anayesema ‘unasemaje?’, harakaharaka nikakwepesha macho yangu, akaondoka zake kwa mbwembwe.
Kimsingi nilikuwa nimechoka mno, ukichanganya na tukio la Khazija ndiyo nilizidi kuchanganyikiwa. Kwa jinsi ninavyomjua mama mwenye nyumba, alichokuwa anakitaka kutoka kwangu hakikuwa mazungumzo wala nini, alikuwa na hasira na mimi kwa yote niliyomfanyia na njia pekee ya kumalizia hasira zake nilikuwa najua anachokitaka.
Nilifunga mlango vizuri na ili kuonesha kwamba sikuwa tayari kwa alichokuwa akikitaka, nilizima kabisa na taa, nikaenda kujilaza kitandani huku mawazo tele yakipita ndani ya kichwa changu.
Japokuwa upande mmoja nilikuwa nimechoka lakini upande mwingine nilikuwa najifikiria, nitaachaje kuitumia nafasi ile ya ofa ya bure kutoka kwa mama mwenye nyumba? Nilisimama na kujaribu kujipima ubavu, nikapiga pushapu mbili tatu, nikaona bado nina nguvu.
Nikarukaruka kidogo, nikaona viungo vinakubali. Nilichokifanya, harakaharaka nilibadili maamuzi, nilivua nguo na kujifunga taulo, nikapulizia ‘air freshner’ maana chumba chote kilikuwa kinanukia manukato ya Ruqaiya! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea.
Baada ya hapo nilitoka na kwenda bafuni kuoga ili kuamsha nguvu mpya, shukrani kwa Mangi kwani ‘busta’ aliyonipa bado ilikuwa ikifanya kazi mwilini. Nilitoka kwa kunyata maana nilijua mwendawazimu Khazija akisikia nafungua mlango anaweza kuja kuliamsha tena dude.
Nilienda mpaka kwenye mlango wa Khazija na ili kuwa na uhakika wa usalama wangu, niliamua kubana komeo la geti lake la chuma kwa nje. Kwa ujanja huo, hata kama angeamka asingeweza kutoka, angalau nikawa na uhakika na usalama wangu.
Nilienda bafuni na kujimwagia maji harakaharaka, nikiwa naendelea kuoga nilisikia mlango wa mama mwenye nyumba ukifunguliwa kisha ukafungwa, nikasikia vishindo nje, nikajua moja kwa moja anaelekea eneo la tukio.
Nilimalizia kuoga na kutoka bafuni, nikaenda mpaka ndani kwangu, tayari alikuwa ameshajaa tele, akawa ananitazama kwa macho yaliyobeba ujumbe mzito.
INAENDELEA
No comments