Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu YaTisa (9)
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kuteremka kwenye gari, nikashuka na vifurushi vya mazagazaga kibao, basi bosi naye alipoteremka, watu karibu wote eneo hilo waliacha kila walichokuwa wakikifanya na kumtolea macho.
Kwa jinsi mwonekano wake ulivyokuwa, alikuwa kiumbe adimu kwenye mazingira kama hayo, basi tukakatiza vichochoro huku kila mtu akiendelea kutushangaa kwa sababu bado ilikuwa ni asubuhi na hatimaye tukawasili nyumbani.
Kwa bahati mbaya, wakati tunafika, mke wa mwenye nyumba ambaye tumezoea kumuita mama Ababuu, alikuwa akifua nguo zake uani, tena kiti chake akiwa amekiweka karibu kabisa na mlango wangu.
Siku zote nilikuwa namheshimu sana mama Ababuu na sikuwahi kumuonesha tabia zozote mbaya, nikaona kitendo cha mimi kuingia na Madam Bella ‘magetoni’, kingemfanya anione kama mtu wa ajabu sana kwa sababu kulikuwa na tofauti kubwa ya kimwonekano na kimwili kati yangu na Madam Bella.
Nilijikaza kiume, nikamsalimu na kufungua mlango huku Madam Bella akishangaa mazingira ya pale, nikamkaribisha ndani ambapo kama ilivyokuwa kwa Nancy, alipoingia tu, alinisifu kwamba chumba changu ni kizuri sana, basi nikamshukuru na kumkaribisha sana.
“Unanikaribishaje hivyo?” alisema huku akitanua mikono yake kama anayesema ‘njoo unikumbatie’. Basi na mimi nilifanya kama alivyotaka, nikaenda na kumkumbatia kwa nguvu, muda mfupi baadaye midomo yetu ilikuwa imegusana, hata sijui nini kilitokea, nilishtukia tu tayari tukiwa kwenye uwanja wa fundi seremala, mara mlango ukagongwa kwa nguvu.
“Ngo! Ngo! Ngooo!”
“Nani tena huyo jamanii,” alisema Madam Bella huku akionesha kukasirishwa sana na kitendo cha mtu huyo kugonga. Niliamka, nikajifunga taulo na kusogea mlangoni, nikafungua kidogo na kuchungulia nje.
“Hivi unajua kwamba ni zamu yako kununua umeme?”
“Ooh! Kumbe zamu yangu imeshafika? Ok, naomba basi nikupe pesa umuagize hata mtoto akanunue.”
“Mtoto gani? Hakuna mtu hapa nyumbani, kama unavyojua wakienda shuleni nabaki peke yangu, hebui nenda kanunue kwa sababu utakatika sasa hivi, tafadhali tusije tukagombana bure,” mama mwenye nyumba alisema huku akiwa ameshika kiuno.
Haikuwa kawaida yake kuzungumza na mimi kwa namna hii, siku zote tulikuwa tukihheshimiana na kama kuna jambo lolote, alikuwa akiniambia kwa ustaarabu lakini siku hiyo alikuwa amebadilika.
Nilibamiza mlango na kurudi ndani, huku nikiwa nimepanda na jazba. Kwa alichokisema, maana yake alikuwa anataka niache kila nilichokuwa nakifanya eti nikanunue umeme, ambao kwanza hata haukuwa umekatika.
Kama hiyo haitoshi, asubuhi hiyo wakati naondoka aliniona sana lakini hakuniambia chochote kwa hiyo kama nisingerudi ingekuwaje? Niliona kama ameamua kunifanyia visa kwa makusudi ili kuniharibia mambo yangu.
“Vipi tena baba’angu,” alisema Madam Bella huku akinishika mkono kwa upole na kunirudisha uwanjani, nikamweleza kilichotokea.
“Usijali, kwani shilingi ngapi?”
“Siyo kwamba hela sina, ninayo lakini asnataka eti nikanunue sasa hivi.”
“Mimi sijakuuliza kama hela unayo au huna jamani mume wangu, mbona unakuwa hivyo,” alisema Madam Bella kwa sauti fulani hivi tamu sana iliyokuwa inatokea kwenye matundu ya pua zake.
Nilipomjibu kwamba ni shilingi elfu tano, aliniambia nisijali, anazo pesa kwenye simu yake kwa hiyo tuendelee na yetu tukimaliza nitampa namba ya luku halafu atanunua. Maelezo yake kidogo yalinifariji na kunirudisha mchezoni.
Haukupita muda mrefu, kipyenga kilipulizwa kuashiria kuanza kwa mpambano wa kukata na shoka, Madam Bella akionesha kukamia sana kuibuka na ushindi wa mapema. Kama kawaida yangu, mpira ulipoanza nilimuacha kwanza atawale mchezo katika dakika za mwanzo.
Kama ilivyokuwa jana yake, Madam Bella alikuwa na pupa sana mchezoni, hata sijui alikuwa na matatizo gani. Alikuwa akicheza kwa kubutuabutua mpira, ilivyoonesha alichokuwa anakitaka ilikuwa ni ushindi wa mapema tu, moyoni nikawa najisemea kwamba hanijui vizuri.
Akiwa ameshaanza kujichokea kutokana na papara zake, nilianza kumuonesha maujuzi kama yale ya mesi, nikawa nakokota mpira kwenye ‘chaki’, nilianza kwa kasi ndogo lakini nikawa naongeza kasi kadiri muda unavyosonga mbele, akawa anapiga ukelele uliozidi kunipa hamasa ya kuendelea kuonesha uwezo.
Nilimpiga chenga dabodabo, nikampiga kanzu na kupiga danadana nyingi na baadaye nilianza kufumua mashuti ya nguvu, haikuchukua muda, akapiga kelele kwa nguvu na kunikaba kama wacheza mieleka, akadondoka pembeni huku akiwa anatetemeka kama amepigwa na shoti ya umeme! Nilikuwa nimemuweza kisawasawa.
“Ngo! Ngo! Ngo,” mlango uligongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Nikainuka pale nilipokuwa nakuchukua tena taulo langu lakini ilibidi nijifute kwanza maana kijasho chembamba kilikuwa kikinitoka, nikafungua mlango na kuchungulia.
“Ina maana nilichokwambia umeona hakina maana au? Kwa nini unakuwa na dharau kiasi hicho Ashrafu? Kwa nini unanidharau kiasi hiki? Au kwa kuwa mimi ni mwanamke,” alisema mama mwenye nyumba kwa sauti ya kutia huruma sana huku macho yake yakibadilika rangi na kuwa mekundu.
Sikuelewa kwa nini amekuwa na hali hiyo, nikashindwa hata nimjibu nini.
“Mimi sitaki kugombana na wewe, naomba ufanye nilichokwambia,” alisema huku akigeuka, akawa anatembea lakini mwendo wake haukuwa ule niliozoea kumuona, ulibadilika na hata nguo aliyokuwa ameivaa, kidogo ilinifanya nitatizike lakini nikahisi kwamba huenda ni kwa sababu alikuwa akifua.
Nilibaki nimeganda namtazama, akapiga hatua kadhaa na kugeuka, macho yangu na yake yakagongana, harakaharaka nikabamiza mlango maana nilijisikia aibu sana hasa ukizingatia jinsi nilivyokuwa namheshimu.
“Kwa nini ametembea vile huku akiwa amevaa khanga moja tu, halafu kwa nini alipofika mlangoni kwake akageuka? Ina maana alijua lazima nitamtazama? Lakini huyu mama mwenye nyumba mbona ananitafutia matatizo?” akili zangu zilikuwa zimehama, nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu pale kitandani.
Madam Bella alikuwa akikoroma, hajiwezi kwa chochote. Kwa sababu mama mwenye nyumba alinisisitiza sana, na Madam Bella alikuwa amelala, niliona ni bora nitoke nje nikanunua umeme mara moja ili nisizidi kumkwaza mama mwenye nyumba.
Nilivaa pensi na singendi, nikachukua shilingi elfu tano kwenye akiba yangu na kutoka nje. Ilibidi nikamgongee mama mwenye nyumba kwa sababu sikuwa na namba ya luku.
“Pita ndani,” alisema, akionekana ni kama kuna kazi alikuwa akiifanya.
Sikuwa na mazoea ya kuingia ndani kwa mwenye nyumba wangu na nakumbuka mara ya mwisho niliingia nilipoenda kulipa kodi ya nyumba tu, kwa hiyo kitendo cha yeye kuniambia niingie kilikua ni zaidi ya mtihani kwangu.
“Ashrafu, ingia tu usiogope,” alisema, nikapiga moyo konde na kuingia. Alikuwa amekaa sebuleni, kwenye kochi la kulala akionesha kuwa na uchovu sana.
“Samahani mama, nilikuwa naomba namba ya luku nikanunue umeme,” nilisema kwa adabu huku nikikwepa sana macho yangu na yake yasigusane maana hata pale kwenye kochi penyewe, alikuwa amelala kihasara sana.
“Ingia hapo kwenye chumba cha watoto, angalia juu ya meza utaona karatasi tulilonunulia umeme mara ya mwisho,” alisema huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa yamebeba ujumbe ambao ulikuwa mgumu sana kwangu kuuelewa.
INAENDELEA
No comments