Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Kumi Na tatu (13)

hadithi nzuri ya kivuruge wa tandale
“Sasa mama, kwa nini tusiende kuyazungumza ndani? Sidhani kama ni sawa kuwapa watu faida.”

“Wewe ndiyo unawapa watu faida, haya njoo huku, mimi sipendi kabisa tabia hizi,” alisema huku akitangulia ndani. Bado alikuwa amevaa vilevile kama nilivyomuacha, akatangulia ndani na mimi nikamfuata.

Tulipoingia tu ndani, harakaharaka alifunga mlango, akanikumbatia na kunibusu kimahaba.

“Kwa nini unakuwa na tabia mbaya kiasi hiki? Kwa nini unatuchanganya?”

“Lakini mama, huyu mimi ndiyo mchumba wangu wa kudumu, nakuomba sana usinifanyie hivi, nakuahidi hutamuona mtu mwingine tofauti na huyu akiingia,” nilimseti, akanibusu tena na bila kujibu kitu aliingiza mkono akamdaka ‘Ashrafu’, kufumba na kufumbua nikashtukia amemuibua kutoka kusikojulikana.

Kwa jinsi alivyotendewa ndivyo sivyo na mwenye nyumba, ‘Ashrafu’ alikasirika na kuvimba kwa hasira, mama mwenye nyumba akanitazama usoni huku akitabasamu, na mimi nikawa namtazama kwa jazba. Alinishika mkono na kuanza kunivutia kule eneo la tukio, nikawa namfuata kama kondoo anayepelekwa machinjioni, mara mlango ukagongwa kwa nguvu!



“Mama Abdul! Mama Abdul,” sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlango ilisikika. Ilikuwa ni sauti ya mwanamke, nikamuona mama mwenye nyumba akisonya kwa hasira, alinielekeza kwa ishara kwamba nikakae kitandani, akatoka na kwenda kufungua mlango.

Sijui alikuwa ni nani na walizungumza nini lakini sekunde chache baadaye, alirudi mbiombio, akautupiliambali upande wa khanga aliokuwa amejifunga na kunivamia mzima-mzima! Ilibidi kila kitu kifanyike harakaharaka kwa sababu niliogopa nikichelewa sana naweza kusababisha matatizo zaidi kwa Nancy.



Kwa kuwa tayari nilikuwa naujua udhaifu wa mama Abdul, mama mwenye nyumba wangu, kipyenga kilipopulizwa tu nilianza mashambulizi ya nguvu, licha ya mwili wake mkubwa, nilimvuruga kisawasawa na ndani ya muda mfupi tu, tayari alikuwa ameshakwea juu kabisa ya mnazi, akaangua dafu na kulipasua, akapiga ‘ukelele’ wa kufurahia maji ya dafu na kudondokea upande wa pili kama mzigo.

Sikutaka kupoteza muda, nilitinga magwanda yangu ‘fasta’ na kutoka, nikimuacha akiwa hana habari kutokana na mchakamchaka wa nguvu niliomkimbiza. Miongoni mwa sifa za kipekee nilizonazo, ni kwamba hata mwanamke awe mbishi kiasi gani, nikishamvuruga kisawasawa lazima apitiwe na usingizi.

Ili kupoteza ushahidi maana mwili wangu wote ulikuwa umelowa chapachapa kwa jasho, nilipitia kwenye mlango mdogo wa nyuma na kutoka nje kabisa, nikaenda mpaka mtaa wa pili na kuingia kwenye duka, nikanunua maji makubwa na kusogea pembeni, nikayagida huku mengine nikinawa usoni na kichwani.

Nilitafuta sehemu na kukaa chini ya mti, nikapigwapigwa na kaupepo mpaka mwili wangu uliporudi kwenye hali yake ya kawaida. Nikainuka na kuelekea kwangu, safari hii nilipitia geti la kawaida na kumbe wakati naingia, Nancy alikuwa akiniona.

“Kwani ulienda wapi tena?”

“Nilienda dukani.”

“Wewe si nilikuona umeingia kwa huyo mwenye nyumba wako?”

“Mbona nilitoka muda uleule, alikuwa anafoka si unajua hawa wameshika sana dini kwa hiyo hawapendi mambo ya kihuni kwenye nyumba yao,” nilimseti Nancy kama kawaida yangu, nikamuona akishusha pumzi ndefu huku akiwa amenikazia macho usoni.

“Kwani hapa ndani kwako ukiacha mimi na huyo unayesema ni mama yako mdogo, nani mwingine huwa anaingia?”

“Hakuna mwingine mpenzi wangu, ni mama mdogo na wewe tu na ndiyo maana leo alipokuona ameanza kunifokea,” nilizidi kumseti, nikashangaa anazidi kunikazia macho usoni.

“Hiyo hapo ni nini?” alisema huku akinioneshea kwa kidole kwenye kona ya kitanda. Ni hapo ndipo nilipoelewa ni kwa nini alikuwa akinitazama sana usoni, nikajikuta nimetahayari mno. Lilikuwa ni kufuli la Madam Bella, kumbe alipokuwa ameenda kuoga, alilifua na kuja kulianika pale bila mimi kujua chochote, nikajua ‘kimenuka’.

Eti na mimi nilijifanya kushangaa kama siamini nilichokuwa nakiona, nikalisogelea lile kufuli na kujifanya nalichunguza.

“Unanifanya mimi mjinga si ndiyo!”

“Hapana Nancy, inawezekana labda mama mdogo ameisahau wakati anaondoka.”

“Hivi unaniona mimi mtoto mdogo si ndiyo?”

“Kweli tena, si unaona kwanza bado mbichi kabisa, yawezekana zile haraka za kuondoka ndiyo akaisahau,” nilizidi kuutetea uongo wangu kwa nguvu zote, Nancy akawa ananitazama kwa macho makavu kama anayetamani hata kuninasa makofi.

“Hebu niambie ukweli, huyu ni mama yako mdogo kweli au mpenzi wako?”

“Kwa nini unakuwa unanihisi vibaya kiasi hicho Nancy? Mimi sina tabia hizo ambazo wewe umeaminishwa kama ninazo! Huyu ni mama yangu mdogo, siwezi kuwa na uhusiano na mwanamke aliyenizidi umri kiasi hiki.”

“Inawezekanaje aweke nguo zake kihasara kiasi hiki kwenye chumba cha mwanaye wa kiume?”

“Una tabia mbaya sana, ningejua upo hivi wala hata nisingekupa nafasi ya kuujua mwili wangu, najutaa,” alisema Nancy huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.

Ilibidi niwe mpole, nikauvaa ule uso wangu wa huruma yaani kama vile nimeonewa sana. Nilichukua mfuko wa rambo na kulitia lile kufuli, nikalifunga na ili kuzidi kumuaminisha kwamba sina makosa, nililiweka juu ya kabati la nguo, nikatoka na kwenda kukaa sebuleni, nikawasha runinga na kuanza kutazama runinga.

Nilitaka apate muda wa kutulia kwanza lakini kubwa, na mimi nipate muda wa kupumzika maana kiukweli pilikapilika za Madam Bella na mama mwenye nyumba zilikuwa zimenichosha mno.

“Mbona nakupigia simu hupokei?” nilisoma meseji kwenye simu yangu. Ilikuwa inatoka kwenye ile namba iliyokuwa ikinipigia kwa muda mrefu tangu nikiwa kwenye Bajaj baada ya kumsindikiza Madam Bella.

Sikutaka kushughulika nayo, nikawa nimejilaza kwenye sofa nikiendelea kutazama muvi, akili yangu ikiwaza namna nitakavyoweza kumtuliza Nancy kwa sababu kiukweli picha lilikuwa limeungua.

Niliutumia muda huo kwenda bafuni kuoga, angalau nikaanza kujisikia vizuri, niliporudi niliendelea kujilaza palepale sebuleni, nikiwa nimejifunga taulo. Sijui nini kilitokea lakini nadhani kwa sababu ya uchovu, nilijikuta nikipitiwa na usingizi mzito palepale kwenye kochi.

Kilichonizindua kutoka usingizini, ilikuwa ni harufu ya pafyumu ya Nancy, kumbe alishakuja na kukaa pale pembeni yangu, mimi nikiwa sina habari. Niliinuka harakaharaka na kukaa vizuri, nikamtazama.

Alijifanya eti yuko bize kuangalia muvi ile niliyokuwa naiangalia mimi lakini tofauti na mwanzo, safari hii alikuwa amevua zile nguo alizokuja nazo na kujitanda upande wa khanga. Licha ya mimi kumtazama, yeye aliendelea kukazia macho kwenye muvi, ikabidi nijiongeze.

“Sijazoea kukuona ukiwa kwenye hali kama hii Nancy, na kitu usichokijua ni kwamba hata ukiwa umenuna, bado unaonekana mrembo sana,” nilimchombeza, akanigeukia na kunitazama usoni. Macho yake yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu nadhani kwa sababu ya kulia wivu.

“Kama nimekukosea naomba sana unisamehe lakini nakuhakikishia hakuna jambo lolote baya nililolifanya, unanihisi vibaya tu,” niliendelea kumbembeleza, safari hii mkono wangu mmoja ukibarizi taratibu kwenye bega lake.

Akawa ananitazama tu bila kusema chochote, basi nilichokifanya, niliinuka na kumshika mkono, nikamuinua, akainuka bila kipingamizi, nikamshika kwa upole, tukaelekea chumbani. Hakuwa mbishi, akawa ananifuata kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.