Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Kumi na nne(14)
Tulipoingia chumbani, niliendelea kumbembeleza kwa sauti ya upole na baada ya dakika kadhaa, alionesha kuanza kuelewa somo, akanikumbatiakwa nguvu huku akilia, akaniambia kwamba ananipenda sana kutoka ndani ya moyo wake, akaniomba sana nisirudie kumuumiza moyo wake.
Muda mfupi baadaye, tayari tulikuwa ‘msambweni’, kama kawaida yangu nikamvuruga kisawasawa kiasi cha kumfanya awe anaweweseka na kuzungumza maneno yasiyoeleweka. Niliutibu kisawasawa moyo wake kiasi cha kuufanya uso wake ambao awali ulikuwa na huzuni, ubadilike na kupambwa na tabasamu laini huku akiwa amefumba macho.
Ili kumdhihirishia kwamba sikuwa nimetoka kufanya jambo lolote baya, tulicheza ngwe zote mbili mfululizo bila kupumzika hata sekunde moja, hali iliyomfanya ajifunge mwenyewe langoni kwake kwa zaidi ya mara tatu mfululizo, akawa hoi bin taabani.
Muda mfupi baadaye, alikuwa akikoroma, usingizi mzito ukiwa umempitia, nikainuka na kwenda sebuleni na kujilaza palepale nilipokuwa nimelala mwanzo, nikaishika tena simu yangu na kukuta kuna meseji nyingine mbili kutoka kwa namba ileile.
“Kwani huyu ni nani?” nilijiuliza huku nikiipiga ile namba, ikaita kidogo kisha nikasikia imepokelewa upande wa pili, sauti nzuri ya kike ikasikika lakini ilionesha aliyepiga alikuwa kwenye kelele nyingi.
“Ashrafu!” aliniita, akionesha kuwa ananifahamu vizuri.”
“Ndiyo mimi, nani mwenzangu!” niliuliza kwa sauti ya chini, nikihofia Nancy asije akaamka kutoka usingizini na kunikuta tena nikizungumza na simu, tena na mwanamke.
“Unanikumbuka?”
“Hapana! Nani mwenzangu?”
“Mimi mpenzi wako, kwani wewe una wapenzi wangapi mpaka usinijue?”
“Mh! Mpenzi wangu yupi?”
“Hahaaa! Nimeamini kweli wewe kivuruge, una wapenzi wengi mpaka unaniuliza mimi ni yupi? Basi mimi naitwa Ruqaiya wa Kariakoo, mpenzi wako mtarajiwa, ushan’fahamu,” alisema mwanamke huyo huku akicheka kwa raha, nikashusha pumzi ndefu baada ya kugundua kwamba kule alikuwa ni Ruqaiya, yule mwanamke mrembo niliyekutana naye kwenye daladala wakati naenda Kariakoo tukakaa naye siti moja.
Moyoni nilifurahi sana Ruqaiya kunipigia kwa sababu ndani ya moyo wangu nilikuwa najihesabia kwamba nimemkosa. Kitendo cha mimi kumuomba namba yake ya simu halafu akakataa na badala yake akataka mimi ndiyo nimpe, kwangu kilimaanisha kwamba nimefeli na nilishajihesabia kwamba nimemkosa.
“Mbona huongei? Limekushuka kivurugee, nimekubamba utamu,” alisema kwa mashauzi huku akiendelea kucheka kwa furaha. Nilishindwa kumjibu chochote kwa kuhofia kwamba Nancy anaweza kunisikia na kuja ‘kuniamshia dude’, nikainuka kwa kunyata na harakaharaka nikatoka mpaka nje.
“Kwa nini umenishtua namna hiyo Ruqaiya jamani,” nilisema nikiwa nyuma ya nyumba, sasa nikiwa na uhuru wa kuzungumza bila hofu ya kusikiwa na mtu yeyote.
“Nimekushtua na nini,” aliniuliza, sauti yake tamu ikawa inapenya mpaka ndani kabisa ya ngoma za masikio yangu, nikaanza kumseti kwa maneno ya kumtoa nyoka pangoni.
Nilimwambia kwamba sikutegemea kama anaweza kunipigia simu kwa hiyo kitendo cha yeye kunipigia muda huo, kilinifanya almanusra nidondoke na kuzimia kwa mshtuko kutokana na jinsi nilivyokuwa namzimikia.
Alicheka mpaka nadhani watu aliokuwa nao jirani wakawa wanamshangaa, hakuweza kuendelea kuzungumza kutokana na kicheko, simu ikakatwa.
Harakaharaka nilimpigia, akapokea huku akiwa bado anacheka, akaniambia eti amemisi vituko vyangu ndiyo maana amenipigia lakini anaomba nisiendelee kuziumiza mbavu zake kwa kicheko.
“Yaani hapa dukani kila mtu ananishangaa ninavyocheka,” alisema huku akikohoa, harakaharaka nikamuuliza kama naweza kuonana naye.
“Unataka kuonana na mimi? Akuu... unataka kunifanya nini?” alisema kwa kudeka, moyoni nikaanza kushangilia ushindi kwa sababu kwanza kitendo cha yeye kupiga simu na kujitambulisha kama mpenzi wangu, baadaye akabadilisha na kusema yeye ni mpenzi wangu mtarajiwa, achilia mbali swali lake hilo la kizushi, niliamini kwa asilimia mia moja kwamba tayari ameshaingia mwenyewe kwenye kumi na nane zangu.
“Nataka nikuone tu jamani, ujue nimesubiri sana simu yako, naomba nikuone leo kama hutajali! Kwani ukitoka kazini una ratiba gani?”
“Naenda zangu nyumbani, namuwahi mwanangu si unajua tena shemeji yako amesafiri kafuata mzigo Dubai kwa hiyo lazima niwahi nyumbani!”
Kauli yake hiyo ilikuwa ni ishara nyingine ya ushindi kwangu, nikaamua kumkomalia hasa baada ya yeye mwenyewe kuniambia kwamba mumewe eti alikuwa amesafiri. Niweke kumbukumbu vizuri, ni kweli nimeshawahi kula viapo vingi siku za nyuma kwamba kamwe siwezi kuangukia dhambini na mke wa mtu!
Tena nilijiwekea na mwiko kabisa lakini nilichokuja kugundua ni kwamba hakuna kitu kibaya kama kujiapiza. Ruqaiya alikuwa ni mwanamke ambaye hata sijui nielezee vipi sifa zake lakini kwa kifupi, uzuri wake ulitosha kabisa kunifanya nivunje viapo vyote nilivyowahi kujiwekea.
Unajua shetani akishakupanda kichwani, hata kama utaambiwa hii ni sumu usiilambe, wewe unaweza kutaka kujaribu uone kama utakufa kweli au laa! Kucheza na Ruqaiya ilikuwa sawa na kucheza na sumu hatari kwa sababu ilishasemwa kwamba mke wa mtu ni sumu, lakini ajabu ni kwamba eti nilijifanya sijali chochote, nikasahau kabisa viapo vyangu!
“Nakuomba sana, utakapotoka kazini unitafute kwa sababu nitakuwepo hukohuko Mtaa wa Aggrey, tafadhali sana naomba nikuone mwenzio,” nilimbembeleza sana Ruqaiya, hakutaka kunikatisha tamaa, jibu alilonipa ni kwamba nisubiri ataangalia kama atapata nafasi ya kuonana na mimi kisha akakata simu.
“Kwisha kazi yake!” nilijisemea huku nikionesha ishara kama ya mchezaji anayeshangilia bao zuri alilolifunga kwenye mechi ngumu, unautingisha mkono kwa nguvu na kuurushia kwa mbele! Kwa wale wacheza soka au mashabiki wazuri wa soka watakuwa wananielewa.
“Ulikuwa wapi?” sauti ya kichovu ya Nancy ilinipokea nilipochungulia tu mlangoni. Kumbe alishaamka na kutoka mpaka sebuleni lakini hakunikuta, akakaa pale nilipokuwa nimekaa, akiangalia muvi.
“Nilikuwa nimeenda hapo dukani mara moja,” nilisema kwa kujiamini, bila kumpa nafasi ya kuzungumza chochote, nikaanza kumpa pole kwa uchovu, alinitazama kwa macho yaliyojaa uchovu, akaachia tabasamu hafifu na kunilalia.
“Unajua nini ninachokihitaji ndiyo maana nakupenda, sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe kwenye maisha yangu, nilikwambia na nitaendelea kukwambia Ashrafu, tafadhali naomba usinitese,” alisema kwa sauti ya kudeka, nikamkumbatia kwa upole na kuanza kumpa maneno matamu, nikimhakikishia kwamba mimi ni wake kwa hiyo asiwe na hofu.
Miongoni mwa sifa mbaya ambayo siwezi kujisifia mbele za watu, ni kwamba nilikuwa muongo sana kwenye mapenzi, na pengine hiyo ndiyo sifa iliyonifanya nifanikiwe kucheza sana na mioyo ya wanawake wengi, jambo ambalo siyo la kujivunia hata kidogo.
Basi nilimdanganyadanganya pale, kwa sababu ya jinsi nilivyomchosha, wala hakutaka tena mpambano uendelee kwa madai kwamba atakaporudi kwao, itakuwa rahisi kwa wazazi wake kumgundua kwamba ametoka sehemu mbaya.
“Hujaniambia kuhusu kilichotokea ulipochelewa kurudi nyumbani.”
“Ni stori ndefu, nitakueleza siku nyingine,” alisema Nancy huku akijilaza vizuri kifuani kwangu. Mara simu yake ilianza kuita, harakaharaka akainuka na kwenda kuichukua.
“Haloo baba! Ndiyo, niko njiani ndiyo nakwenda baba,” alisema kwa unyenyekevu, nikawa namtazama nikiwa na shauku kubwa ya kusikia anazungumzia nini. Alipokata simu, huku akionesha kutofurahishwa na simu hiyo, alinisogelea na kwa upole akaniambia:
“Samahani mpenzi wangu, ujue asubuhi baba alikuwa ameniagiza kwamba nikamchukulie dawa zake Muhimbili halafu yeye atamtuma mtu aje kuzichukua kazini kwangu, si nimesahau mwenzio.”
Sijui alitegemea kwamba nitakasirika baada ya kunieleza hivyo au ni vipi, lakini kwangu mimi hizo zilikuwa ni habari njema.
“Si utanisindikiza?”
“Hapana baby, naomba sana unisamehe kwa hilo, kazini nimedanganya kwamba naumwa, kitendo cha mimi kuonekana huko mitaani kinaweza kuniletea matatizo,” niliingizia uongo mwingine, akanielewa kwa haraka bila kipingamizi chochote.
INAENDELEA
No comments