Chombezo : Kivuruge Wa Tandale Sehemu Ya Kumi Na Moja (11)
“Mungu wangu!”
“Vipi?”
“Huyo anayepiga hodi.”
“Amefanyaje?”
“Hata sijui nikueleze vipi unielewe! Unaweza kunisaidia kitu? Naomba utoke ukamwambie kwamba sipo, akikuuliza wewe ni nani mwambie ni mama yake mdogo umetokea Zanzibar,” nilisema huku nikitetemeka maana kulikuwa na kila dalili kwamba hatimaye naenda ‘kugonganisha matreni’.
“Hivi wewe unanifanya mimi mtoto si ndiyo?”
“Hapana Madam, wala siyo hivyo! Fanya kwanza halafu nitakufafanulia ni nini kilichotokea, utacheka mwenyewe,” nilimseti, akanitazama usoni kama anayetaka kupata uhakika kuhusu jambo fulani kisha kinyonge aliamka na kujifunga upande wa khanga, akaenda kufungua mlango.
“Shikamoo!”
“Marahaba hujambo?”
“Sijambo, samahani nilikuwa namuulizia kaka Ashrafu.”
“Hayupo, ameenda kazini! Wewe ni nani?”
“Naitwa Nancy, ni rafiki yake tulisoma wote. Basi akija utamwambia namtafuta naona nampigia simu hapokei. Wewe n nani yake?”
“Mimi! Usijali utanijua siku nyingine,” nilimsikia Madam Bella akimjibu Nancy kwa sauti isiyo rafiki kisha akabamiza mlango kwa nguvu na kumuacha Nancy akiwa bado amesimama pale nje.
Nadhani baadaye aliamua kuondoka kwa sababu nilisikia vishindo vyake akiondoka, nikainuka na kwenda kuchukua simu yangu ambayo tangu nifike nilikuwa nimeiweka kwenye chaji. Kulikuwa na ‘missed calls’ na meseji kibao lakini kabla hata sijaangalia ni nani aliyenipigia au kunitumia meseji, Madam Bella tayari alikuwa ameshafika.
Hakutaka kuzungumza chochote na mimi lakini usoni alionesha kuwana hasira, sijui alihisi nini huko nje, nikawa namsubiri aanze kunihoji. Hata hivyo, hakunihoji chochote, alichokifanya ilikuwa ni kuangusha ule upande wa khanga pembeni, kile ambacho Nancy alikivuruga kikaanza upya.
Tofauti na mara ya kwanza, safari hii alionesha ni kama amenikamia kwa sababu kwanza uso alikuwa ameukunja na hata namna alivyokuwa akitandaza soka, rafu zilikuwa nyingi na alikuwa akitumia nguvu kwa makusudi.
Nilichokigundua ni kwamba alikuwa na hasira lakini kwa kuwa alikuwa akihitaji huduma yangu ya ‘ufundi wa kompyuta’, aliamua kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, yaani apate huduma lakini wakati huohuo pia anioneshe hasira zake.
Wale waliosema hasira za mkizi furaha kwa mvuvi hawakukosea, nilijiweka katika ‘engo’ fulani hivi ili amalize vizuri hasira zake, basi akawa anabutua mashuti ya nguvu, wakati mwingine ananilima daruga kwa makusudi, mimi nikatulia mchezoni.
Nikawa naendelea kumjibu kwa pasi murua na mashuti ya hapa na pale, chenga za maudhi na wakati mwingine nikawa nakimbia na mpira kwenye chaki. Yeye aliendelea kupiga mashuti ya nguvu na mimi nikawa namkabili vilivyo, taratibu zile ndita alizokuwa amekunja kwenye uso wake zikaanza kufutika, akafumba macho halafu akawa ni kama anataka kupiga chafya na kucheka kwa wakati mmoja.
Hata sijui nini kilitokea, alinibana kifuani kwa nguvu, akawa ni kama ananibusu kwenye kifua changu cha mazoezi mara nikashtukia amening’ata kwa nguvu huku akipiga yowe kama mtu aliyeibiwa mkoba na simu yake Kariakoo.
Nilijisikia maumivu makali pale kifuani lakini nikajikaza kiume, akawa anatetemeka kama aliyepigwa na shoti ya umeme na safari hii alianza kuangua kilio huku akilitaja jina langu, muda mfupi baadaye akadondokea pembeni akiwa hajitambui.
Kama nisingewahi kukikaza kifua changu huenda pale aliponing’ata angeniumiza sana lakini aliishia kuniachia alama. Haukupita muda mrefu akaanza tena kukoroma! Nilichokigundua kwa Madam Bella, hakuwa na stamina kabisa, yaani akishakwea mpaka juu ya mnazi na kuangua dafu, basi alikuwa akiishiwa kabisa nguvu na kupitiwa na usingizi mzito.
Ni hapo jdipo nilipopata muda wa kuchukua simu yangu na kuangalia ni nani na nani waliokuwa wakinipigia. Nilishtuka kugundua kwamba miongoni mwa watu walionipigia sana simu, alikuwa ni Nancy lakini pia Salma naye alikuwa amenipigia.
Mbali na kunipigia, Nancy kumbe alikuwa amenitumia na meseji, kwa ilivyoonesha ni kama alianzia kazini kwa sababu kulikuwa na meseji aliyoniambia kwamba nipo hapa nje tulipokuwa tumekaa jana, njoo mara moja! Meseji zilikuwa nyingi na kumbe mpaka anakaribia pale nyumbani alikuwa akinitumia meseji na kunipigia bila majibu yoyote.
Huwa nina kawaida ya kuiweka simu yangu ‘silent’ kwa hiyo ni mpaka niwe nayo mkononi ndipo ninapoweza kugundua kama kuna mtu ananipigia, nikishaiweka pembeni tu, basi kila kitu kinaharibika.
“Mwanaume muuaji sana wewe! Yaani kumbe unaishi na jimama kwako ndiyo maana hata simu zangu hupokei?” meseji mpya iliingia kwenye simu yangu, nikashtuka kidogo maana ilikuwa inatoka kwa Nancy.
“Sasa leo siondoki, nitakusubiri hapa kwako hata kama ni mpaka usiku wa manane, nipo hapa dukani,” meseji nyingine iliingia kutoka kwa Nancy, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kutafakari nini cha kufanya.
Shughuli za mapishi zilikuwa zimesimama kwanza, Madam Bella akawa anaendelea kukoroma kwa nguvu. Nilichokifikiria ni kwamba lazima nimtengenezee mazingira Madam Bella aondoke zake maana niliona kama ananikosesha uhuru.
Sikutaka kwenda naye kwa pupa, nilimuacha apumzike wakati mimi nikiwa nimejilaza kwenye kochi nikiendelea kutafakari namna ya kumpanga Nancy mpaka anielewe. Nilijua nitakapomtumia meseji yoyote, lazima atapiga na mazingira niliyokuwepo nisingeweza kupokea simu yake. Nilifikiria kutoka na kwenda kuzungumza na simu nje lakini kwa kuwa alishaniambia kwamba yupo hapohapo jirani, ningeweza kukutana naye na kukosa majibu ya kumpa, nikaona njia nzuri ni kuuchuna.
Basi dakika chache baadaye, Madam Bella aliamka, akajizoazoa na kuja pale nilipokuwa nimejilaza, akanikumbatia na kunibusu huku akionesha bado kuwa na usingizi mzito.
“Utaniua mwenzio ujue,” alisema kichovu, wote tukacheka. Nilimwambia kwamba njaa inaniuma kwa hiyo amalizie kupika, alichinijibu kilinifanya nicheke tena.
“Siwezi hata kusimama, utamalizia mwenyewe kupika.”
“Sasa tutakula nini?”
“Kanunue hata chipsi, siwezi kufanya chochote,” alisema huku akinibusu tena. Akaniambia kwamba eti nimemuudhi sana kwa sababu inaonekana pale kwangu wasichana wengi huwa wanakuja.
“Hapana, hawa ni marafiki tu! Wewe kwanza ni shahidi kwamba muda mwingi huwa nakuwa kazini, sasa huwa wanakuja saa ngapi?” nilianza kumtengeneza kwa maneno laini.
INAENDELEA
No comments